Monday, September 14, 2015

Huduma ya Tigo Pesa iliyoboreshwa yarahishisha ufanyaji miamala kwa wateja

Wateja wa kampuni ya Tigo sasa wanaweza kutuma na kupokea fedha kupitia simu zao za mkononi kirahisi na kwa haraka kutokana na maboresho makubwa ambayo kampuni hiyo imefaniyia huduma yake ya Tigo Pesa.

Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Tigo jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya habari ikisema kwamba maboresho hayo pia yamerahisiha ulipiaji wa ankara za huduma mbalimbali ikilinganishwa na ilivyokuwa kabla.

“Tunayofuraha kuwatangazia wateja wetu kwamba baada ya zoezi la maboresho kukamilika kwa ufanisi sasa huduma za  Tigo Pesa zimerejea,” ilisema taarifa hiyo. Huduma za Tigo Pesa zilisitishwa usiku Jumamosi, Septemba 12 hadi Jumapili mchana, Septemba 13 ili kufanya majaribio ya maboresho ya mtandao.

Tigo Pesa ni huduma maarufu ya kifedha ikiwa na wateja zaidi ya milioni nne  nchini kote.

Huduma zinazotolewa na Tigo Pesa ni kutuma na kupokea fedha miongoni mwa wateja wa Tigo na kwa wateja wa mitandao mingine ya simu, kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti ya simu kwenda benki na kutoka kwenye akaunti ya benki kwenda simu ya mkononi, kulipia huduma mbalimbali.



Mwaka jana Tigo ilikuwa kampuni ya kwanza duniani kuanzisha huduma ya kutuma na kupokea ya kimatifa kwenda nchini Rwanda baina ya watumiaji wa Tigo Pesa nchini na Tigo Cash nchini Rwanda. Tigo pia ilikuwa ya kwanza mwaka 2014 duniani kuanza kulipa faida kwa watumiaji wa Tigo Pesa kutokana na kiasi cha amana kilichoko katika akaunti ya mteja. Malipo haya hufanyika kila baada ya miezi mitatu

No comments: