Thursday, September 17, 2015

JESHI LA POLISI NA WADAU WAHIMIZA UCHAGUZI HURU NA WA HAKI


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinindoni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Camillius Wambura  ameitaka jamii kushiriki katika uchaguzi mkuu wa October 25, 2015 katika hali ya utulivu ili kukuza democrasia na kuwezesha uchaguzi huo kuwa huru na wa haki. 
Amesisitiza hayo katika kikao na wadau wa uchaguzi kilichoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na asasi ya  Hanns Seidel Foundation (HSF) uliofanyika katika ukumbi wa maafisa wa Polisi Oysterbay, Kinondoni jijini Dar es Salaam

"Uchaguzi huru na wa haki wenye kuzingatia democrasia  ni muhimu na hauepukiki kwani ni nyenzo muhimu katika kuandaa msingi imara wa maendeleo ya taifa hili". alisema Kamanda Wambura.

HSF na Jeshi la Polisi waliandaa kongamano hilo kujadili  ni namna gani jamii iamasishwe kushiriki  katika ujao kwani uchaguzi wa kidemocrasia ni chachu ya maendeleo, na endapo uchaguzi huo usipoendeshwa kwa umakini machafuko na vurugu vinaweza kuibuka na hatimaye kuzorotesha maendeleo ya nchi hii.

Kongamano hilo limeendeshwa kufuatia maboresho yanayoendelea ndani ya Jeshi la Polisi katika mradi wake wa Polisi Jamii unaohusisha mashauriano, kutatua changamoto, pamoja na mambo mengine. Aidha, hii ni fursa kwa Jeshi la Polisi kuwa na uelewa wa pamoja na wadau wa uchaguzi na jamii kwa ujumla katika kubaini changamoto za kiusalama, kijamii na kiuchumi ka kuweka mpango wa pamoja katika kutanzua changamoto hizo.

"Ni fursa nzuri kwa wadau muhimu kama viongozi wa madhehebu ya dini, vyama vya siasa, watu wenye ushawishi katika jamii, na Taasisi zisizo za kiserikali: kuhimiza, kutia moyo, na kuonyesha uhalali wa wajibu huo kuelekea huru na wa haki".  amesema EMMANUEL MALILA - Mkurugenzi Mtendaji wa TASODEMO (Taasisi inayojihusisha na uchambuzi wa masuala ya kisiasa na Kijamii),

Aidha, kongamano hilo limewawezesha washiriki kupata ufahamu juu ya masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na haki za binadamu, mchakato wa uchaguzi mkuu, makosa ya uchaguzi, haki na wajibu wa vyama vya siasa, sheria ya vyama vya siasa, mikutano ya hadhara, vyama vya siasa katika chaguzi za kidemokrasia, kampeni sahihi, na madhara ya watu kutokufuata sheria katika mchakato mzima wa uchaguzi mkuu.  

The participants lastly agreed with resolutions to be worked upon, which will be a catalyst to community; the participants included: Assistant returning officers, religious leaders, political parties leaders, Non-Governmental Organizations, Civil based Organizations, Faith based Organizations, Influential personnel ,Law enforcement organs, Media industry, Youth group (Bodaboda group) and Local Government Authorities.

washiriki wa kongamano hilo ni pamoja na viongozi wa madhehebu ya dini, viongozi wa vyama vya siasa, taasisi zisizo za kiserikali,  mashirika ya kijamii, watu maarufu, vyombo vya ulinzi na usalama, wanahabari vikundi vya vijana (bodaboda) na Mamlaka ya Serikali za Mitaa.  

No comments: