Friday, September 25, 2015

KAMPUNI YA SIMU YA TIGO NA REACH FOR CHANGE WAZINDUA SHINDANO LA WAJASIRIAMALI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa shindano la Wajasiriamali ambapo ametoa wito kwa watu kushiriki ili wajiweke katika nafasi ya kushinda fedha taslimu dola za kimarekani 20,000 ambazo kila mshindi atapewa azitumie katika utekelezaji wa mawazo yao ya kibunifu.
  Meneja wa Reach for Change nchini Tanzania, Peter Nyanda, akizungumza katika mkutano huo.
 Muasisi wa Mfuko wa APPS and Girls, Carolyne Ekyasisiima, akizungumza jinsi mfuko huo unavyofanyakazi ya kusaidia watoto katika masomo.
 Mwanzilishi wa Shule Direct, Iku Lazaro akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Ni furaha tupu kwenye uzinduzi huo.
 Meneja wa Mawasiliano wa Tigo, John Wanyanca akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Bw.Suleiman Khamis(alieavaa miwani) mmiliki wa blogu ya Bongo Daily updates akifuatilia uzinduzi huo, pembeni ni mmiliki wa blogu ya Mwanaharakati mzalendo bw.Krantz Mwantepele
 Mkutano wa uzinduzi huo ukiendelea.
 Madada hawa wenye fulana za uzinduzi huo wakifuatilia matukio yote kwa karibu 'Wamependeza'
Hawa ni baadhi ya wanafunzi walionufaika na mradi huo.

Tigo na Reach for Change wazindua shindano la wajasiriamali jamii


Kila mshindi kupokea dola za kimarekani milioni 20,000 kwa ajili ya utekelezaji Dar es Salaam, Seeptemba 25, 2015. Tigo kwa kushirikiana na taasisi ya Reach for Change zimezindua shindano wajasiriamali jamii liitwalo “Tigo Digital Change-makers” lenye lengo la kuibua mawazo ya kibunifu ambayo yatasaidia kutatuta matatizo yanayowakabili watoto na vijana nchini.


Meneja mkuu wa Tigo Diego Gutierrez leo ametangaza uzinduzi wa shindano hilo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam ambapo ametoa wito kwa watu kushiriki ili wajiweke katika nafasi ya kushinda fedha taslimu 

dola za kimarekani 20,000 ambazo kila mshindi atapewa azitumie katika utekelezaji wa mawazo yao ya kibunifu.

 “Tigo ikishirikiana na Reach for change itatoa tuzo ya dola za kimarekani 20,000 kwa kila mmoja kwa washindi wawili ambao watakuwa na mawazao bunifu zaidi kiteknolojia na kidijitali yaliyo na uwezo wa kuchangia kuleta  maisha bora kwa watoto katika jamii ya kitanzania,” alisema Gutierrez.


Aliongezea kwamba, “Lengo letu ni kupata mawazo ya kibunifu ya kidijitali ambayo yataleta na kutatua matatizo yanayowakabili watoto kwa kiwango kikubwa huku tukiendelea kuwekeza katika kukuza na kuimarisha huduma zetu za mawasiliano katika maeneo yote nchini.”


Mawazo yatakayowasilishwa kupitia shindano hili yanatakiwa kuonyesha uwezo wa kutumia simu kidijiti tekinolojia ya habari na mawasiliano kuleta ufanisi wa utekelezaji wa mradi husika. Watakaopenda kushiriki shindano hili wanaweza kutuma maombi kupitia mtandao wa www.tigo.co.tz/digitalchangemakers, kwa mujibu wa Gutierrez.


Kwa upande wake, Meneja wa Tanzania wa Reach for Change,Peter Nyanda, alisema licha ya kupata kitita cha dola 20,000 washindi pia watapewa vifaa vya kuendeleza utekelezaji wa mawazo yao ikiwa ni pamoja na kupata ushauri kutoka kwa 

wafanyakazi waandamizi kutoka Tigo na Reach for Change. Aidha wataunganishwa na wajasiriamali wengine ambao tayari wamenufaika kutokana na mpango huo.

Mchakato huu wa kuwapata wajasiriamali jamii wa kidigitali unaendana na mkakati wa Tigo wa kuendeleza maisha ya kidijitali nchini. Huu ni mwaka wa nne mfulilizo ambapo taasisi za Tigo na Reach for Change zimekuwa zikishirikiana kuwasaidia wajasiriamali nchini. Jumla ya wajasiriamali watano wamenufaika na mpango katika kipindi hiki ambao kwa pamoja na kupitia utekelezaji wa miradi yao wamewasaidia jumla ya watoto zaidi ya 10,000 nchini.


Mwisho

No comments: