Wednesday, September 30, 2015

Miezi Mitano sasa Tazara Hawajalipwa mishahara,Muda huu Wameamua kukutana,soma hii


 Wafanyakazi wa  Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) leo wameibuka na kudai kuwa sasa ni miezi motano hawajui wala kuonja ladha ya mshahara huku kukiwa hakuna maelekezo wala kauli yoyote kutoka serikalini jambo ambalo limezua taharuki kubwa ndani ya mamlaka hiyo na kusababisha wafanyakazi wa shirika hilo kukutana kujadili hali hiyo inayowakumba.


Mtandao huu umekutana na mkutano uliokuwa unafanyika ndani ya mamlaka hoyo ulioitishwa na chama cha wafanyakazi wa reli nchini Tanzania TRAWU kikiwashirikisha wafanyakazi wote wa mamlaka hiyo ambapo mada kuu katika mkutano huo ni kujadili hali ngumu waliyonayo ambapo wamesema kuwa hadi sasa  ni mwezi wa tano hawajapata mishahara yao huku wakiwa wamelalamika serikalini bila majibu ya kuridhisha.
Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa Reli nchini TRAWU Bwana MUSA KALALA akizngumza wakati wa mkutano unaoendelea sasa Hapa Tazara Baina ya chama hicho na wafanayakazi lengo lao ni kudai mishahara yao
Mwenyekiti wa chama hicho MUSA KALALA amezungumza na mtandao huu kuhusu madhumuni ya mkutano huo ambapo amesema kuwa lengo lao sasa ni kupaza sauti yao kuhusu mishahara  ili serikali iweze kuwasikiliza na kuwasaidia.
Bwana MUSA amesema kuwa huu ukiwa ni wakati wa uchaguzi ni lazima serikali itambue kuwa wafanyakazi wa shirika hilo ni wapiga kura,na wanawahudumia wapiga kura hivyo kuwanyima haki yao kwa muda mrefu kunaweza kusababisha matatizo makubwa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Ameongeza kuwa kumekuwa na matatizo makubwa yanayowakumba wafanyakazi wa mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja na wengine kufukuzwa kazi au kusimamishwa kutokana na kuonekana wanadai haki yao kwa kasi mbele ya jamii jambo ambalo amesema sasa uongozi wa chama hicho unaliangalia ili waliofukuzwa waweze kurejea kazini mara moja.

No comments: