Wednesday, September 16, 2015

MPE RIZIKI SIO MATUSI,ACHA KUWADHALILISHA WANAWAKE MAENEO YA BIASHARA

Wasanii wa vikundi mbalimbali vya sanaa za maigizo wakinyesha namna wanawake wanavyodhalilishwa kwa vipogo katika maeneo mbalimbali ya bishara na hata katika famililia leo katika tamasha maalum liloloandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la EQUALITY FOR GROWTH (EFG) Tamasha lililofanyika katika soko la Sterio Temeke Jijini Dar es salaam.Picha na Exaud Mtei
 Imeelezwa kuwa maeneo ya masokoni,migodini na sehemu zenye matengenezo ya barabara ndizo sehemu zinazoongoza kwa udhalilishaji wa wakiina mama hasa kwa njia ya matusi na udhalilishaji wa kingono kwa wanamama hao.

Hayo yamebeinika leo jijini Dar es salaam wakati wa Tamasha maalum lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la EQUALITY FOR GROWTH (EFG) shirika ambalo linajishughulisha na utetezi wa haki za kijinsia katika maeneo ya biashara tamasha ambalo limefanyika katika soko la sterio Temeke jijini Dar es salaam kwa lengo la kutoa elimu kwa watanzania wa eneo hilo juu ya unyanyaswaji wa wanawake katika maeneo ya biashara  na jinsi ya kuchukua hatua.
SUSAN SITTA ambaye ni Afisa mradi wa kampeni ya MPE RIZIKI SIO MATUSI inayoendeshwa na shirika hilo akizngumza  na wananchi na wafanya biashara wa Soko la sterio Temeke Jijini Dar es salaam katika tamasha hilo
Katika kampeni inayoendeshwa na shirika hilo iliyopewa jina la MPE RIZIKI SIO MATUSI ina lengo la kupita katika mawnwo mbalimbali kutoa elimu kwa wafanya biashara hasa wakina mama jinsi ya kuepuka mambo ambayo yanawadhalilisha wakiwa kazini na hasa jinsi ya kutumia sheria ambazo zipo ili kujilinda na kadhia hiyo ambayo imetajwa kuendelea kuenea katika maeneo mengi ya biashara hapa Tanzania.
Afisa Tathmini na Ufwatiliaji wa shirika hilo SAMORA JULIUS akizngumza na wakazi wa Temeke na wafanyabiashara wa soko hilo waliojitokeza kwa wingi kupata Elimu juu ya unyanyasaji wa wanawake unaotokea katika maeneo ya masoko na maeneo mbalimbali ya Biashara.
Akizungumza wakati wa Tamasha hilo Afisa Mradi wa kampeni hiyo ya MPE RIZIKI SIO MATUSI,Bi SUZAN SITTA amesema kuwa maeneo ambayo tafiti za shirika hilo zinaonyesha kukithiri sana kwa udhalilishaji wa wanawake katika maeneo ya biashara ni pamoja na maeneo ya masoko,maeneo ya migodi,pamoja na maeneo ambayo kumekuwa kukifanyika shughuli mbalimbali kama maeneo ya ujenzi wa bara bara.
Anaeleza kuwa matusi,udhalilishaji wa kingono,kudharaulika ni moja ya kadhia nyingi ambazo wamekuwa wakikutana nazo katika maeneo mengi ambayo shirika hilo limekuwa likifanya ziara huku akikiri kuwa hali hiyo kuendelea kuwa kubwa kutokana na kutokuwa na nia dhabiti ya kutoa elimu kwa wahusika juu ya tabia hiyo.

Wakazi waliohudhuria katika Tamasha hilo la Temeke leo wamekiri kuwepo kwa maswala hiyo katika soko la Sterio Jijini Dar es salaam ambapo wengi wao wamesema kuwa sababu kubwa ya udhalilidhaji wa wanawake kazini unatokana na wanaume wengi kutokuwaheshimu wanawake ambao wanafanya kazi mfano za mama Ntilie,wauza matunda,pamoja na bishara nyingine katika soko hilo ambapo wameomba wahusika kuendelea kutoa elimu pamoja na kuchukua hatua za kisheria.

Wadau mbalimbali wa kampeni hiyo wakiwemo pia wa wafadhili kutoka UN-GENDER wakiwa wanashiriki katika Tamasha hilo la kutoa elimu juu ya unyanyaswaji wa wanawake juu ya wanawake sehemu za Biashara
Aidha wamesema kuwa tabia hiyo inakuwa na madhara makubwa sana wa kwa wahusika ikiwa ni pamoja na kushusha heshima zao,kutokujiamini wakiwa kazini,pamoja na kushindqwa kiufanya biashara kwa kuhofia kadhia hiyo kuwakumba.
Shirika hulo limekuwa liktimbelea maeneo mbalimbali ya masoko ambapo kwa lengo la kutoa elimu juu ya unyanyaswaji wa wamnawake katika maeneo ya biashara na jinsi ya kujikinga na kadhia hiyo
HAMAD JUMA mwenyekiti wa soko la STERIO TEMEKE akiiangumza na wakazi waliojitokeza katika Tamasha hilo
Burudani ilikuwa ni sehemu ya kazi hiyo,Chinio unaweza kuangalia picha nyingi za tukio nzima leo


























No comments: