Sunday, September 6, 2015

TAMASHA LA NYAMA CHOMA FESTIVAL LATIKISA DAR ES SALAAM


DJ akiwarusha mashabiki na wapenzi wa kinywaji cha HEINEKEN waliohuduria jana katika tamasha la nyama choma festival lililofanyika katika viwanja vya LEADERS Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na mashabiiki na wadau mbalimbali kutoka kila kona ya Jiji .
Tamasha Maarufu nchini Tanzania linalokutanisha idadi kubwa yawatanzania kwa sasa Tamasha la NYAMA CHOMA FESTIVAL limefanyika Jana katika viwanja vya leaders club Jijini Dar es salaam chini ya udhamini mkubwa wa bia bora kwa sasa nchini na duniani bia ya HEINEKEN ikiwa ni mwaka wa pili sasa kudhamini Tamasha hilo.

Tamasha hilo ambalo liliandaliwa na Alta Vista Events na  indulged ilishughudiwa mashabiki na watanzania waliohudhuria wakipata burudani ya aina yake kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiwemo Bend maarufu ya music nchini FM ACADEMIA,Pamoja na wasanii wa kizazi kipya AY,na MWANA FA.

 Meneja wa HEINEKEN nchini Tanzania Bwana Michael Mbungu akizungumza na mtandaso huu wakati wa Tamasha hilo alisema kuwa Bia yao inajivunia sana kuwa moja katimya wadhamini wa Tamasha kubwa kama hilo nchini huku akisema kuwa udhamini wa matukio mbalimbali ni moja wa mkakati wao wa masoko ili kuendelea kuwa na ushirikiano wa karibu sana na wadau ambao ndio wateja wao wa kila siku.
Alisema kuwa moja ya sababu kubwa iliyowavutia wao kama HEINEKEN kuweka udhamini wao katika Tamasha la NYAMA CHOMA FESTIVAL ni kutokana na ubora na umakini wa tamasha hilo pamoja na ushirikiano mkubwa wanaoupata kutoka kwa Kiongozi na mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa tamasha hilo,Carol Ndosi ambapo amesea kuwa lengo kuu ni kuleta starehe kwa watanzania kwa njia ya kuwajibika
Wadau na wapenzi wa Kinywaji cha HEINEKEN waliokuwa wanaendelea kupata burudani ya aina yake katika viwanja hivyo.

 Aidha mkurugenzi mtendaji wa Alta Vista Events Carol Ndosi akizungumza na mtandao huu amesema kuwa moja ya mikakati ya Tamasha hilo Tangu kuanzishwa kwake ni kuhakikisha kuwa linavuka nje ya Tanzania na kufika katika nchi za Africa mashariki ambapo amesema kuwa mkakati huo unaendelea kufanyiwa kazi.

Alisema kuwa Tamasha hilo limekuwa na mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake ikiwa ni pamoja na kufanikiwa kuleta watanzania wengi pamoja na kuwa na mapenzi na nyama choma na kuendelea kutoa Burudani mbalimbali kwa watanzania ambao wamekuwa wakihudhuria Tamasha hilo
Bend maarufu ya FM ACADEMIA wakitoa burudani viwanjani hapo.

No comments: