Muslim Hassanali, Mgombea ubunge jimbo la ilala kwa Tiketi ya CHADEMA na kuungwa mkono na UKAWA STORY NA OPTATUSY STAN-DAR ES SALAAM |
Wakati kampeni za
uchaguzi mkuu zikiwa zimepamba moto katika maeneo mbalimbali nchini chama cha Demokrasia
na maendeleo chadema katika manispaa ya ilala kimewataka wakazi wa manispaa
hiyo kukipa ridhaa ya kumchagua mbunge
wake anayekiwakilisha ili kiweze kuwaletea maendeleo.
Hayo yamesemwa na mzamini
wa chama hicho Bw Alkado Ntagazwa wakati wa mkutano wa chama hicho wa kumnadi
mgombea wa chadema anayeungwa mkono na
umoja wa vyama vinanyounda ukawa Bw HASSANARI maarufu kama ROFA WA ILALA uliofanyika katika viwanja vya soko la karume
jijini Dar es salam,
Bw ntagazwa amesema
kuwa wananchi wa eneo hilo hawapaswi kukosea tena na kukichagua chama cha mapinduzi
kwa kuwa kimewaletea umasikini mkubwa ambao wanauona hadi sasa.Bw ntagazwa
aliwambia wakazi wa eneo hilo kuwa miaka ya nyuma elimu ilitolewa bure kwa watu
wote kwanini isiwe sasa? Bw ntagazwa alihoji.
Ntagazwa amewaomba
wakazi wa manispaa ya ilala kutokosea kama ambavyo uwa wanafanya miaka
mingine.Kwa upande wake mwenyekiti wa wa
vijana wa chama cha chadema Bw mwita amesema kama wananchi wa eneo hilo
wataamua kukipigia kura chama chake katika nafasi zote watakuwa wamejiondoa
kwenye matitizo mabalimbali kama kitendo cha kufukuzwa mara kwa mara na mgambo
wa jiji kwenye maeneo yao ya kufanyia shughuli zao.
Mwita alibainisha kuwa
watanzania wengi wana maisha magumu huku akiwataka polisi waache kutumika na
badala yake wasimamie kanuni na taratibu za utekelezaji wa majukumu yao tofauti
na ilivyo sasa Kwa upande wake mgombea wa ubunge wa jimbo hilo bw Hassanari
amesema kuwa uwa anajisikia vibaya sana pale anapoona kuwa wakazi wa emeo hilo
wananyanyasa na mgambo wa jiji huku wakiwa na uhalali wa kuishi kwa uhuru na
haki katika maeneo yao.
Bw Hassanali ameongeza kuwa jambo la kwanza
atakalolifanya kama atapewa ridhaa na wana ilala ni kuhakikisha kuwa fedha za
maendeleo zinawafikia walengwa bila kuguswa na wajanja wachache.Huku
akishangiliwa na wafanyabiashara na wananchi waliohudhuria mkutano huo bw
hassanari alijinasibu kuwa yeye ndo muarobaini wa matatizo yote ya wakazi wa
eneo hilo hivyo wana ilala hawakiwi kufanya makosa tena katika uchaguzi wa
mwaka huu
No comments:
Post a Comment