Friday, September 4, 2015

Watanzania washauriwa Kutumia kinywaji cha TREVO

Mark Stevens( Katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na bidhaa ya Trevo katika Hotel ya Serena jijini Dar es salaam.kushoto kwake ni David Kagoro na kulia ni Michael Ajao ambao wote ni wawakilishi wa kampuni hiyo nchini Tanzania
 Rais na Mwanzilishi wa kampuni inayotengeneza kinywaji chenye virutubisho  ya Trevo Bw.Mark Steven yupo nchini Tanzania kuangalia jinsi kinywaji chake kinavyoenea nchini  huku akiwahimiza watanzania kutumia kinywaji cha Trevo chenye virutubisho takribani 174 katika mwili wa binadamu.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo Mark amesema kwamba Kinywaji cha Trevo ni kinywaji kilichotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu uliohusisha  vyakula mbalimbali nyenye kiwango kikubwa kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Bidhaa hiyo imethibitishwa na mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA pamoja na Shirika la Viwango nchini (TBS),Kinywaji hicho kinasambazwa nchini kwa njia biashara ya Mtandao ambapo hadi sasa ni zaidi ya wanachama elfu tatu wamejiunga nchini Tanzania.
Muonekano wa kinywaji hicho
Mkurugenzi huyo anataraji kutembelea katika mikoa minne ya Dar es salaam,Mwanza,Arusha,Mbeya ambapo mikoaa hiyo kuna maduka ya kiinywaji hicho ambacho amekitaja kama kinywaji bora ambacho kina uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali katika mwili wa binadamu 
Kufuatia mahitaji kuwa makubwa kampuni  hiyo inatarajia kufungua tawi lingine mkoani Mbeya siku ya jumatatu Sept 7,2015 ambapo inasambazwa pia katika mikoa ya Dar es salaam, Arusha  na mkoani Mwanza.

No comments: