Thursday, October 15, 2015

Goli la mkono----Madudu Makubwa Daftari la wapiga kura,Tizama yaliyoibuliwa leo na CHADEMA

Mwanasheria kutoka CHADEMA Bwana JOHN MALLYA akionyesha baadhi ya vifungu vya sheria ambavyo vinaruhusu wapiga kura kukaa meter mia mbili kulinda kura zao
 Katika hali ya kushangaza baada ya Tume ta uchaguzi kusambaza nakala ya daftari la kudumu la wapiga kura kwa vyama vya siasa jana jioni hatimaye madudu makubwa yameanza kubainika ndani ya daftari hilo jambo lililozua taharuki kubwa kwa vyama kadhaa huku wakiwa hawana imani na daftari hilo tena.
Picha za wapiga kura kutoka kituo cha Dodoma Mjini ambazo zipo kmwenye daftari la kudumu la wapiga kura lililotolewa na Tume hiyo Huku picha nyingine zikiwa hazina wahusika zikiwa na giza na majengo
Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA wamekuwa wa kwanza kujitokeza mbele ya wanahabari baada ya kuanza kulikagua daftari hilo na kuonyesha madudu makubwa ambayo wamedai yanafanyika na tume hiyo kwa ajili ya kukisaidia chama tawala kiweze kuendelea kuwa madarakani.


Akizungumza na wanahabari mchana wa leo Mkurugenzi wa uchaguzi kutoka chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA Bwana REGNAD MUNISHI ameeleza mambo ambayo yamejitokeza ndani ya daftari hilo ambayo ni ya kushangaza ikiwemo kuwepo kwa picha ambazo hazina sura za watu zikiwa na giza,kuwepo kwa picha za majengo ambazo zimepewa vitambulisho,Picha za watu wawili kwenye Picha moja,picha za wachina,na picha ambazo hazina mandhari yanayofanana kwa kituo kimoja,jambo ambalo amedai ni utani mkubwa na hato yote ni katika kituo kimoja ndani ya Dodoma mjini nab ado wanaendelea kufanya upembuzi juu ya daftari hilo.
Mkurugenzi wa uchaguzi wa CHADEMA REGINALD MUNISHI akifafanua jambo
Akizugumza huku akionyesha picha kadhaa ambazo zimepigwa kwenye kituo kimoja cha Dodoma Mjini MUNISHI amesema kuwa kituo kimoja kimekutwa na makosa zaidi ya 17 yote yakiwa ni ya makusudi na yanayoweza kuhatarisha uchaguzi na kuhitimisha kauli ya goli la mkoni katika uchaguzi huo.


SWALA LA KULINDA KURA.
Wakati mijadala nchini Tanzania kwa sasa ikiwa nji swala la nani anaruhusiwa kukaa karibu na vituo baada ya kupiga kura kwa kile kinachoitwa kulinda kura,umoja wa katiba ya wananchi UKAWA umeibuka na kusisitiza kuwa sheria ya uchaguzi ya mwaka 1985 inamruhusu mpiga kura yoyote kukaa meter mia mbili kutoka kwenye kituo cha kupiga kura hivyo kauli za vitisho zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa chama tawala na serikali ni kauli za mfa maji na haziwezi kuwatisha katika harakati zao za kusaka mabadiliko nchini Tanzania.
Makamu Mwenyekiti CHADEMA akifafanua jambo
Wakizungumza na wanahabari leo makamu mweyekiti wa CHADEMA Pofesa ABDALA SAFARI pamoja na mwanasheria kutoka CHADEMA Bwana JOHN MALLYA wamesema kuwa hakuna sheria inayomkataza mtanzania kulinda kura yake na kusisitiza kuwa sheria ya uchaguzi inasisitiza kuwa kukaa meter mia mbili kutoka kituo cha kupigia kura na sio vinginevyo.

Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania DK JAKAYA KIKWETE akiwa sherehe za kuzima mwenge mjini Dodoma kupiga marufuku kukaa karibu na vituo vya kupigia kura huku akisema kuwa kwa atakayekiuka hilo atakumbana na nguvu kubwa ya vyombo vya dola.


Baada ya maamuzi hayo ya serikali kutangazwa jana na serikali UKAWA kupitia kwa makamu mwenyekiti nwa CHADEMA Profesa SAFARI amesema kuwa baada ya maswala hayo yanayoendelea katika uchaguzi huo wameamua kuandika barua haraka za malalamiko kwa jumuiya za kimataifa ikiwemo mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC pamoja na jumuiya za madola kulalamikia kile ambacho wanakiita rafu ya uchagfuzi  inayofanywa na chama tawala ili kisitoke madarakani.
Picha moja watu wawili
Kiongozi huyo anasema kuwa kauli ya Rais KIKWETE ya vitisho ukilinganisha na madudu ambayo yanaoneka katika daftari lililotolewa jana inaonyesha wazi kuwa kuna michazo michafu inayochezwa na seriukali ili kupingana na nguvu ya mabadiliko njambo ambalo wamesema kuwa hawatakubaliana nalo

 PICHA NYINGINE ZINAENDELEA CHINI----



No comments: