Kauli Ya lowasa kuhusu kifo cha DEO FILIKUNJOMBE

Ni taarifa ya kushtusha sana ya msiba wa mwanasiasa chipukizi na jasiri, Deo Filikonjombe kutokana na ajali ya Helikopta jana jioni maeneo ya mbunga ya Selous mkoani Morogoro.

Ni pigo lingine kubwa ambalo katika kipindi kifupi Taifa limepata, huku bado likiwa na kidonda cha kuondokewa na wana siasa wengine mahiri,Marehemu Celina Kombani, Dr Abdallah Kigoda na Dr Emanuel Makaidi aliyefariki jana
Filikonjombe alikuwa Mbunge mahiri aliyesimama imara kutetea maslahi ya wananchi wa jimbo lake la Ludewa na watanzania kwa ujumla.

Alikuwa mwiba kwa serikali ya Chama chake CCM kutetea maslahi ya nchi, mfano ni katika kashfa ya Escrow ambapo alikuwa Makamu Mwenyekiti wa kamati iliyochunguza kashfa hiyo.

Mwenyezimungu awape moyo wa subira, familia, jamaa, marafiki na wananchi wa Ludewa, katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.-Edward Ngoyai Lowassa

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.