Kufwatia kifo cha
mwanasiasa mkongwe na mwanaharakati wa siasa za Tanzania ,Mwenyekiti wa chama
cha DP mchungaji Cristopher Mtikila kilichotokea juzi kwa ajali ya Gari,baraza
la vyama vya siasa nchini wametangaza kuahirishwa kwa kikao cha baraza kuu la vyama
vya siasa nchini kilichokuwa kifanyike tarehe 6 na 7 mwezi wa kumi visiwani
Zanzibar hadi tarehe itakayopangwa tena
baada ya maziko ya marehemu mchungaji MTIKILA.
Akizungumza na
wanahabari Jijini Dar es salaam leo Mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa
nchini Tanzania PETER KUGA MZIRAY amesema kuwa kamati ya uongozi ya baraza la
vyama vya siasa kwa niaba ya baraza hilo wameshtushwa sana na kifo cha
mwanasiasa huyo na wamekutana kwa dharura na kuamua kusogeza mbele kikao hicho
ambacho kinatajwa kujadili mambo muhimu na nyeti kuelekea uchaguzi mkuu wa
mwaka huu.
“Kifo cha mchungaji
MTIKILA ni pengo kubwa sana katika siasa na democrasia ya vyama vingi nchini
kwani amekuwa mdau mkubwa katika kudumisha na kuboresha mfumo wa siasa za nchi
yetu na democrasia ya vyama vingi hapa nchini”amesema mziray.
Aidha baraza hilo
limetoa salamu za rambi rambi na pole nyingi kwa wanafamilia ya marehemu
wanachamawa DEMPCRATIC PARTY (DP) na ndugu na jamaa wote,na kuwataka wawe na
moyo wa uvumilivu kwani kila mtu anaondoka duniani kwa namna na siku yake.
Mchungaji mtikila
alifariki siku ya jumapili alfajiri katika ajali ya gari iliyoacha njia na
kupinduka mkoani pwani wakati akiwa safarini kuelekea jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment