Saturday, October 17, 2015

MAGUFULI aweka historia MWANZA,Tizama hii

Dkt. Magufuli (katikati) akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Nyamagana (pichani kulia) Ndugu Stanslaus Mabula mbele ya Maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Furahisha jioni ya leo.Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza waliohojiwa na Globu ya Jamii walieleza na kukiri wazi kuwa haijawahi kutokea kwa mapokezi haya makubwa na ya aina yake,na kuwa Magufuli ndiye anaetosha kuvaa viatu vya Urais.

 Dk Magufuli (katikati) akiwanadi Mgombea Ubunge Jimbo la Ilemela, Anjela
Mabula 
Dk Magufuli (katikati) akiwanadi Mgombea Ubunge Jimbo la Ilemela, Anjela
Mabula na Stanslaus Mabula ambaye anagombea ubunge Jimbo la Nyamagana.

Maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake wakiwa wamekusanyika mithili ya Utitiri kwenye uwanja wa Furahisha jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni,ambapo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia na kuwaomba wampigie kura za kutosha ifikakapo Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia  Maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake katika viwanja vya Furahisha jioni ya leo jijini Mwanza kwenye mkutano wa kampeni,ambapo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia na kuwaomba wampigie kura za kutosha ifika Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.
 Wananchi
wakiuzuia msafara wa Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Pombe Magufuli  uliokuwa ukisindikizwa na umati wa watu kutoka Uwanja wa Ndege
wa Mwanza kwenda kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Furahisha
jijini Mwanza.

 Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John pombe Magufuli ukiondoka katika viwanja vya Furahisha jioni ya leo mara baada kumaliza mkutano wa kampeni,huku ukisindikizwa na umati mkubwa wa watu.
PICHA NA MICHUZI JR-JIJINI MWANZA.

No comments: