Mtandao wa asasi za
kiraia wa kuangalia uchaguzi nchini Tanzania TACCEO umelaani vikali kitendo cha
jeshi la polisi kuvamia kituo cha ukusanyaji wa matukio mbalimbali yaliyokuwa
yanajili wakati mchakato wa uchaguzi ulipokuwa unaendelea na kuchukua baadhi ya
vifaa vya kituo hicho na kuwakamata baadhi ya maafisa wake.
Akizungumza na
waandishi wa habari mapema leo KAIMU MWENYEKITI WA UMOJA HUO BW HEBLON
MWAKAGENDA amesema kuwa tukio hilo lilitokea octoba 29 majira ya saa nane
katika eneo la mbezi bichi eneo ambalo kituo hicho kilikuwepo.
Bwana Mwakagenda
amebainisha kuwa wakiwa kazini walishuhudia gari ya jeshi ya polisi ambayo
ilikuwa na polisi sita waliokuwa wamevaa mavazi ya kujihami pamoja na silaha za
moto wakiingia kituoni hapo ambapo askari hao walianza kuchukua vifaa vyao
mbalimbali walivyokuwa wanafanyia kazi zikiwemo kompyuta za mezani 25,kompyuta
mpakato 3 simu 25 za ofisini na kuwakamata waanglizi wao 36.
Aidha Bwana Mwakagenda
ameeleza kuwa matukio ambayo yanafanywa na jeshi la polisi yanatakiwa kulaaniwa
na kila mpenda Demokrasia maana yanalenga katika kudhoofisha demokrasia nchini
ambayo ndo msingi wa utawala bora
Wanahabari wakichukua Taarifa hiyo |
Hata hivyo BW
MWAKAGENDA ameitaka selikali kutotumia
vyombo vya dola katika michakato yeyote ya kidemokrasia kwani kwa kufanya hivo
kunaweza kuleta uvunjifu wa amani iliyojengwa kwa mda mrefu.
Ameongeza kuwa swala
hilo limetokea huku vyombo vya dola vikitambua wazi kuwa uangalizi huo wa
uchaguzi ulifwata misingi yote iliyowekwa kikatiba na sheria pamoja na kuwa na
vibali na vitambulisho maalum kutoka tume ya uchaguzi vilivyowaruhusu kufanya
kazi hiyo kihalali.
Kaimu mkutugenzi wa LHRC ambao ni wataribu wa mtandao huo IMELDA LULU URIO akizungumza katika mkutano huo |
Akizngumza na
wanahabari katika mkutano huo Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na haki za
binadamu nchini Tanzania LHRC ambao ndio waratibu wa mtandao huo Bi IMELDA LULU
URIO amesema kuwa tukio la kuvamiwa kwa waangalizi wao na jeshi la polisi sio
la kwanza kwani wakati waangalizi hao wakifwatilia zoezi la uandikishwaji wa
daftari la kudumu la mpiga kura kwa mfumo wa BVR huko Njombe waangalizi wao
walivamiwa na polisi na kupigwa wakiwa katika kazi zao na hadi leo hakuna
ufafanuzi wowote uliotolewa na mamlaka husika kuhusu chanzo cha tukio hilo.
No comments:
Post a Comment