Mgombea udiwani katika kata ya mbagala Kuu akimwaga serera mbele ya wakazi wa Mbagala katika viwanja vya Zakiem jioni ya leo |
Mgombea Udiwani Kata ya Mbagala Kuu kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM ,
Yusuphu Manji amewataka vijana
wasidanganywe na mabadiliko na kudai
kuwa fedha zake nyingi zitatumika kwa
ajili ya kuleta maendeleo.
Akizunguza katika
mkutano wa Hadhara wa kuomba ridhaa ya wana mbagala kuu amesema kuwa endapo atapewa ridhaa ya kuwa Diwani katika Kata hiyo
atahakikisha anachimba visima vingi ili kutatua changamoto ya maji ambayo
imekuwa sugu katika maeneo hayo kwa sasa.
Manji ambaye katika
upande wa michazo ni mwenyekiti wa timu ya Yanga ameahidi kuwa endapo atapata
ridhaa kila mwaka katika Kampuni zake
atawapatia vijana ajira huku akiahidi
pia kuongeza Zahanati na kuboresha
huduma za afya katika kata hiyo.
Aidha katika hatua
nyingine mgombea huyo ameahidi kujitolea kuwakopesha wanachi hao magari zaidi
ya 20 kuzoa taka katika maeneo hayo ikiwa ni jitihada za kupambana na tatizo la
usafi katika kata hiyo
Pia Manji aliongeza kuwa atawawekea wananchi wake
sola,ndani ya miaka miwili ataboresha miundo mbinu shuleni huku swala la mifuko
ya wakina mama atasimamia fedha zinazotengwa
ili waweze kukopeshwa waendeshe
biashara zao.
Katika upande mwingine
naye MGOMBEA Ubunge wa jimbo jipya la
mbagala Mbagala jijini Dar es Salaam,Ally Mangungu amesema endapo wananchi
watampa ridhaa ya kumchaguwa atahakikisha anajenga Chuo Cha Ufundi Stadi ili vijana waweze kujiajiri na kuweza
kufikia ndoto zao.
Akizungumza jijini Dar
es Salaam Katika mkutano wa kampeni za
Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika viwanja vya Zakhem,Mangungu amesema
hapa nchini kumekuwa na wimbi la vijana ambao hawana ajira hali
inayowasababisha wajiunge katika vitendo vya uvunjifu hivyo Chuo hicho
akikijenga kitasaidia kupunguza wimbi
la umaskini linalowakabili
vijana.
Amesema Chuo hicho kitakapojengwa kitawawezesha
kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji na kuwawezesha kujitegemea na kufikia malengo yao ya maisha.
“Mbali na kujenga Chuo
hicho, ntahakikisha najenga aliahidi atajenga shule ili wanafunzi wanapomaliza
kidato cha nne waweze kujiunga na kidato cha tano na sita:
MGOMBEA Ubunge wa jimbo jipya la Mbagala Mbagala jijini Dar es Salaam,Ally Mangungu akizngumza katika mkutano huo |
Nakuongeza kuwa jimbo hili lina shida ya vyumba vya madarasa ntahakikisha tunapata madarasa ya
kutosha”alisema Mangungu.
Akizungumzia wanawake
amesema atahakikisha anafuatilia Sh.
Million 10 zinazotengwa kila mwaka na Halmashauri ya Manspaa ya Ilala ili
wanawake wakopeshwe waweze kuendesha biashara zao.
No comments:
Post a Comment