Tuesday, October 27, 2015

Sentens TATA za wakuu wa UKAWA jioni hii mbele ya wanahabari


Wenyeviti wa umoja wa katiba ya wananchi UKAWA wakiongozwa na mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo chadema ambaye ni mbunge mteule wa jimbo la Hai pamoja na mwenyekiti wa NCCR mageuzi ambaye poa ni mbunge mteule wa jimbo la vunjo pamoja na makamu mwenyekiti wa cha cha democrasia na maendleo chadema Profesa ABDALA SAFARI jioni ya leo wamezungumza na wanahabari kuhusu maswala mbalimbali aambayo yanajitokeza kipindi hiki cha utangazaji wa matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Tanzania,Hapa nimejaribu kukunukulia baadhi ya maswala muhimu ambayo wamezunguzia hapo.-------------



MBOWE---Huu haukuwa uchaguzu ulikuwa ni uchafuzi na vita kubwa sana,haukuwa uchaguzi wa huru na haki.

MBOWE—Kwanini majimbo ambayo wagombea wetu wameshinda inakuwa ni vigumu sana kwa matokeo kutangazwa hadi itokee mabomu na nguzu kubwa sana ndipo matokeo yatangazwe,pilisi wanajaribu kulazimisha matokeo ambayo wanayajua wao wakishirikiana na wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa ambao wote wanajaribu kukisaidia chama cha mapinduzi.

MBOWE—Hatuyatambui wala kuyapokea matokeo ambayo yanatangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi kuhusu kura za urais kutoka katika majimbo mbalimbali,matokeo hayo hayaendeni hata kidogo na ukweli wa mambo na wala hayafanani hata kidogo na Form ambazo sisi tunazo kutoka kwa mawakala wetu hatuyataki.

MBOWE—Vijana wetu na wataalamu wa IT ambao walikuwa wanafanya kazi halali kabisa ya kiukisaidia chama kupata matokeo kutoka kwa mawakala wetu kote nchini na kuyajumlisha ili wawee kulinganisha na matokeo ambayo yanatolewa na tume,wamekatwa toka juzi vijana zaidi ya 160,wamevamia center yao,wameharibu mifumo yao ya upokeaji wa kura na kuvunja baadhi ya vifaa vyetu vya kufanyia kazi hiyo.

MBOWE—Wamewagawanya vijana hao katika vituo mbalimbali vya polisi wengine jana wamepelekwa segerea kukaa huko na tumepata taarifa kuwa vijana wengine walikuwa wanapelekwa mahakama ya kisutu jioni hii na tumefika pale ni kweli vijana wetu nane wamefikishwa pale na wamefunguliwa mastaka ya makosa ya mtandaoni jambo ambalo ni lakushangaza kweli.

MBOWE—Hii sio haki kwani vijana hao walikuwa wanafanya kazi halali kabisa,wakati huo huo CCM wao vijana wao ambao wapo HYJAT HOLEL jijini Dar es salaam na tunajua wapo wanafanya kazi hiyo hiyo na JANUARY MAKAMBA kila siku anatangaza matokeo wanayopokea ila wao wanaonekana hawana kosa lolote ila wakifanya ukawa ni CYBER CRIME.

MBOWE—Kwa misingi hiyo sasa tumeamua kuwa,kesho tukutane kamati kuu ya chadema ikiwa ni kamati kuu ya dharura kujadili nankuamua nini kifanyike baada ya uchaguzi huu kuharibika wazi wazi,na kesho hiyo hiyo pia tutakutana summit ya viongozi wakuu wa vyama vya UKAWA kujadili na kutoa maamuzi ya maswala haya.

MBATIA—Huu sio uchaguzi ni vita kubwa sana,kwa mfano juzi kule vunjo Kilimanjaro nililala nje tukipita kukusanya masanduku yaliyokuwa yamefichwa majumbani mwa watu yakiwa na kura za Rais wa CCM na tukakamata mengi sana ila tumepeleka polisi baadae wakakanusha na kusema kuwa hakuna jambo lililotokea bali ni masanduku ya tume  yalikuwa yakipekewa katika vituo.

MBATIA—Lengo letu kama ukawa ni kudumisha amani ya Tanzania,tunafanya haya yote ili kuokoa taifa hili lisije likaingia katika machafuko ya aina yoyote.


MBATIA—Namaliza kwa kusema hivi unaweza kuchakachua kura ila huwezi kuchakachua hisia za watanzania.Asanteni


Katika  tamko  lake, Profesa  Safari  ametolea  mfano  jimbo  la  tandahimba  ambapo  amesema, kwa  mujibu  wa  matokeo  yaliyotangazwa  na NEC  katika  jimbo   hilo,Magufuli amepewa kura  49,098 huku  Lowassa  akiambulia  46,288

Kwa  mujibu  wa  Profesa  Safari, matokeo  halisi  waliyoyakusanya  toka  kwa  mawakala  wao  yanaonyesha  kuwa  Magufuli  ana  kura  44,253   huku  Lowassa  akiwa  na  kura 44,537

No comments: