·
MAJAMBAZI SUGU SITA WALIOMMUA AFISA WA POLISI ASP
ELIBARIKI PALLANGYO WAKATWA. WAPATIKANA NA SILAHA MBILI.
·
WATUHUMIWA WA UGAIDI WAZIDI KUKAMATWA KATIKA
OPARESHENI KALI INAYOENDELEA. SABA WASHIKILIWA POLISI KANDA MAALUM. PIA
ZIMEKAMATWA BUNDUKI NNE NA RISASI18
jeshi la Polisi kanda maalum ya dar es salaam
wamefanikiwa kuwakamatwa majambazi sugu sita walioshiriki katika mauaji ya ASP
Elibariki Palangyo huko nyumbani kwake Yombo Makangarawe tarehe 04.08.2015.
waliokamatwa ni: 1) OMARY SALEHE@BONGE MZITO (39)
MKazi wa Mtoni mtongani ambaye ni Kiongozi wa kundi hilo
2) SAIDI SAIDI MAZINGE (37) Mkazi wa Tegeta
Kibaoni
3)
RASHIDIWATSONB@ DODO(21) MKAZI WA Vingunguti
4)RAMADHANI SALUM@NGUZO 38 mkazi MBAGALLA
KIBURUGWA
5) BAKARI SALIM RASHIDI@ MALENDA (38) Mkazi wa
Mbagala kizuiani
6) HAMISI HAMISI @ FREEMASON 24 Mkazi wa Mbezi
Mwisho
Afisa huyo wa ngazi ya juu katika jeshi la Polisi
alikuwa anafanya kazi Mkoani Morogoro katika kikosi Maalum cha kupambana na
majambazi aliyekuja nyumbani kwake Dar Es salaam. Alikuja DSM kwa ajili ya
kusalimia familia na ndipo alipovamiwa na majambazi usiku wa manane wakati
amelala na familia yake.
Aidha mtuhumiwa
namba mmoja alikutwa na silaha bastola aina ya revolver iliyofutwa namba
na baada ya mahojiano. aidha mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa ni marehemu kabla
ya kufariki alijaribu kuwatoraka askari kwa kukimbia alijeruhiwa na hatimaye
alifia njiani wakati akipelekwa hosptalini. Pia inasemekana marehemu
alipotezana na familia yake miaka mitani iliyopita akiwa kwenye harakati ya
ujambazi.
Pia bonge mzito alikuwa akitafatwa na Polisi kwa matukio mazito ya ujambazi
wa kutumia silaha na mauaji ambaye pia amehusika katika mauaji ya afisa wa
Polisi nyumbani kwake usiku wa manane na kumuua mbele ya familia yake
ikishuhudia.
Pia mtuhumiwa RASHIDI WATSON@ DODO alikamatwa
maeneo ya Vingunguti tarehe 01.10.2015 akiwa na silaha aina ya Shortgun
ilikatwa mtutu na kutengenezwa kienyeji ikiwa na risasi nne na betri mbili
zilizounganishwa kwa ajili ya kulipua baruti.
Watuhumiwa wengine watano watapelekwa mahakamani
baada ya kuperuzi na kukamilika kwa
upelelezi wa shauri hilo.
WATUHUMIWA
WA UJAMBAZI WANAOJIHUSISHA WANAOJIHUSISHA NA UGAIDI WAPATAO SABA WAKAMTWA, SITA KATI YAO NI WAFIMILIA
MOJA
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaamkwa
kushirikiana na mikoa ya jirani pamoja na vyombo vingine vya dolalimeendelea
kufanya oparesheni ya kuwatafuta na kisha kuwakamata wale wote wanaojihusisha
na matukio ya kupanga na kuvamia vituo vya Polisi, kuua askari/raia kisha
kupora silaha jambo linaloashiriavitendo vya kigaidi.
Oparesheni hiini kali na ya aina yake kwa
madhumuni ya kukomesha kabisa vitendo vya uvamizi wa vituo vya Polisi na wale
wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine lazima wakamatwe ili sheria
uchukue mkondom wake. Oparesheni hii pia ina lengo la kuwaondolea hofu wananchi
dhidi ya vitendo vya kigaidi nchini na kwamba wananchi waendelee kutoa taarifa
juu ya watu kama hao ili nchi yetu iendelee kuwa na amani na utulivu.Majina ya
watuhumiwa waliokamatwa ni kama ifuatavyo:
1. SIAD S/O MOHAMED ULATULE @ USO WA SIMBA, Miaka 67,
Mkazi wa Mandimkongo, Mkuranga mkoa wa Pwani.
2. RAMADHANI S/O ALLY NGANDE, Miaka 29, Dereva wa
Bodaboda, Mkazi wa Kongowe.
3. HAMIS S/O MOHAMED SALUM SIMBA ULATULE, Miaka 51,
Mkulima, Mkazi wa Mamdimkongo, Mkuranga, Pwani.
4. ALLY S/O MOHAMED SALUM SIMBA ULATULE, Miaka 65, Mkulima,
Mkazi wa Mamdimkongo, MKuranga, Pwani.
5. NASSORO S/O SELEMAN ULATULE, Miaka 40, Mkulima,
Mkazi wa Mamdimkongo, Mkuranga, Pwani.
6. SELEMAN S/O ABDALLAH SALUM ULATULE, Miaka 83,
Mkulima, Mkazi wa Mamdimkongo, MKuranga, Pwani.
7. SAID S/O ABDULLAH CHAMBETA @ Mzee wa Fasta, Miaka
40, Mfanyabiashara wa Mitumba, Mkazi wa Yombo Makangarawe.Mtuhumiwa namba 1,3,4
na 5 ni wa familia moja inayojihusisha na vitendo vya ujambazi pamoja na vya kigaidi.
Tunawashukuru sana watanzania wazalendo na wenye
mapenzi mema na nchi yao kwa kutoa ushirikiano wa hali na mali ambao umesaidia
kupata mafanikio yote haya.Tunawaomba waendelee kulisaidia Jeshi la Polisi kwa
kuendelea kutoa taarifa ili oparesheni hii iwe yenye ufanisi zaidi.
KUKAMATWA
KWA BUNDUKI SMG MOJA NA SHORTGUN MBILI, BASTOLA MOJA PAMOJA NA RISASI 14.
Katika
hatua nyingine, Jeshi la
Polisi linamshikilia mtuhumiwa MUSSA S/O MALAKI AKUTI, Miaka 30, fundi wa
magari, Mkazi wa Mbagala Charambe kwa kukutwa na bunduki aina ya “Chinese 56 SMG” yenye namba 563845189 ikiwa na magazine moja na risasi 14. Mtuhumiwa huyu alikamatwa
tarehe 28/09/2015 maeneo ya Mbagala Sabasaba, Temeke jijini Dar es Salaam baada
ya Polisi kupokea taarifa kutoka kwa raia wema.
Bunduki hiyo ambayo aliiweka chini ya kiti cha
pikipiki aina ya BOXER yenye namba T269 AUX inayosemekana kutumika katika
matukio ya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.Upelelezi
unaendelea ili kuwakamata watuhumiwa wengine ili sheria iweze kuchukua mkondo
wake kutokana na
No comments:
Post a Comment