Baraza la wazee la chama cha Democrasia na maendeleo
CHADEMA leo wamepongeza uamuzi wa kada maarufu na mkongwe wa chama cha
mapinduzi KINGUNGE NGOMBALE MWIRU uamuzi wa kukiacha chama chake cha CCM na
kujiunga na harakati za watanzania za kusaka mabadiliko huku wakisema ni
maamuzi ya kishujaa na yanayopaswa kupongeza na kila mtanzania mpenda
mabadiliko.
Akizungumza na wanahabari mapema leo Jijini Dar es
salaam katibu wa baraza hilo Bwana RODERICK LUTEMBEKA amesema kuwa maamuzi na
kauli alizozitoa mkongwe huyo ambaye anatajwa kuwa ni mmoja wa waasisi wa
chama cha mapinduzi ni za kweli na za wazi kwani chama alichokuwepo kinaonekana
wazi kuwa kimeshindwa kuwasaidia watanzania na kama mwanasiasa anayeakisi
mabadiliko ni hatua sahihi kukihama chama hicho.
Bwana LUTEMBEKA amesema kuwa kauli aliyoitoa
kingunge kuwa chama cha mapinduzi kimeishiwa pumzi ni kauli sahihi kwani Chama
hicho kimeshindwa kusikiliza na kutatua kero za watanzania huku akisema kuwa
chama hicho hakiwezi tena kuepuka mabadiliko ambayo watanzania wengi
wanayahitaji kwa sasa.
Ameongeza kuwa watanzania sio siri tena wanahitaji
mabadiliko pamoja na hofu kubwa ambayo wamekuwa wakijazwa na vyama vingine kuwa Tanzania
haiwezekani bila CCM jambo ambalo amelikanusha na kusema kuwa nchi ya Tanzania inaweza
kuendelea kustawi bila uwepo wa CCM ndani ya uongozi wa Tanzania.
Amesema kuwa maneno ya kingunge kuwa chama cha
mapinduzi kimeishiwa pimzi lakini ni zaidi ya kuishiwa pumzi ni chama ambacho kinakwenda
kufa kutokana na kushindwa kuwahudumia watanzania ambao walikipa dhamana zaidi
ya miaka 50 sasa.
No comments:
Post a Comment