Tuesday, November 24, 2015

CAF YAENDESHA SEMINA YA LESENI ZA VILABU


Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Yahya Hamad leo amefungua semina ya mafunzo ya leseni za vilabu katika ukumbi wa mikutano wa Dar es salaam International Conference Centre (DICC) uliopo jijini Dar es salaam.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Yahya amesema imekua jambo jema kwa CAF kutupatia nafasi ya mafunzo ya leseni za vilabu hapa nyumbani, kwani viongozi wa vilabu wote wanapata nafasi ya kushiriki semina hii ya siku mbili kutoka kwa wakufunzui wa CAF.
“Uendeshaji wa mpira wa miguu duniani umebadilika, mabadiliko haya yapo katika nyanja zote za uongozi (utawala), miundombinu, kitu ambacho kwa sisi Tanania tumeshaanza kuendana na mabadiliko hayo, na sasa kupata kwetu semina hii kutawafanya viongozi wengi kufahamu umuhimu wa leseni za vilabu na kufanyia kazi mapungufu yaliyokuwepo” alisema Yahya.
Semina hiyo ya Leseni kwa Vilabu itakayofanyika kwa siku mbili inaedeshwa na wakufunzi watatu kutoka CAF ambao ni Dr. Bolaji Ojo Oba (Nigeria), Amanze Uchegbulanm (Nigeria) na Othman Mohamed kutoka nchini Sudan.

Agizo la CAF ni kuwa kila klabu inayoshiriki michuano ya kimataifa (Ligi ya Mabingwa, Kombe l Shirikisho) lazima iwe imepata leseni hiyo ambayo itaipa nafasi ya kushiriki michuano inayoandaliwa na CAF, na kwa klabu ambayo haitatimiza mahitaji ya kupata leseni hiyo haitaweza kushiriki michuano ya kimataifa.
Ili kupata leseni ya klabu, klabu inapaswa kutimiza vigezo vilvyowekwa ikiwemo masuala ya utawala, ripoti ya mapato na matumizi iliyokaguliwa, uwanja wa mazoezi nk.
Mmiliki mmoja wa klabu hatarusiwa kumiliki timu zaidi ya moja kwenye ligi moja, kila klabu lazima iwe na program za vijana na uwanja wa mazoezi.

No comments: