Wakati hali ya kisiasa
visiwani Zanzibar ikiwa katika sintofahamu kubwa baada ya uchaguzi kufutwa
hatimaye aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF na mwanasiasa mkongwe
Profesa IBRAHIM LIPUMBA leo ameibuka na kupinga maamuzi ya kufutwa kwa uchaguzi
huo huku akiitaka tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC kuendelea na mchakato wa
kumtangaza mshindi wa uchaguzi huo mara moja.
LIPUMBA ameyasema hao leo
jijini Dar es salaam katika ofisi za chama cha wananchi CUF Buguruni ikiwa ni
mara ya kwanza kwa mawanasiasa huyo kuonekana mbele ya wanahabari tangu
kujiuzulu kwake kulikotokana na kutokubaliana na maswala kadhaa ya kisisa yaliyokuwa
yanaendelea katika umoja wa katiba ya wananchi UKAWA.
Lupumba Akizngumza na wanahabari kuhusu hali ya kisiasa nchini baada ya uchaguzi |
Amesesma kuwa kitendo
cha mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar kufuta uchaguzi wa visiwa hivyo
na kuitisha uchaguzi mpya ni maamuzi batili kwani kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar
na ya Tanzania tume hiyo haina mamlaka ya kufuta uchaguzi hivyo akamtaka
mwenyekiti wa tume hiyo JECHA SALUM JECHA kutafakari maamuzi yake ambayo
ameyaita ni maamuzi ya kushinikizwa na kisha kuendelea na mchakato wa uchaguzi
huo ikiwemo kumtangaza mshindi halali wa uchaguzi huo.
“Ni jambo la kushangaza
sana kuona kuwa kura za Zanzibar ambazo zimemuweka magufuli madarakani
zinaonekana ni halali laikini uchaguzi wa zanzibari unaitwa kuwa ni uchaguzi
batili hii haiingii akilini,haiwezekani pia uchaguzi ulienda vizuri na
mwenyekiti huyo alianza kutangaza matokeo ya uchaguzi huo kwa majimbo
mbalimbali,lakini baada ya kuona kuwa matokeo hayo yanakiegemea chama Fulani basi
amefuta uchaguzi na kuamu kuitisha uchaguzi mwingine hii ni aibu kwa taifa”Amesema
mwanasiasa huyo ambaye ni mchumi maarufu Africa.
Lipumba ambaye leo
alijitambulisha kama mtanzania mzalendo amemtaka Rais wa sasa wa Zanzibar Dk
ALLY MOHAMEID SHEIN kukubali matokeo halali ya kura na kukabidhi nchi kwa
mshindi kwani kushindwa kufanya hivyo kutaiingiza nchi hiyo katika machafuko
makubwa ambayo yatagharimu roho za wazanzibar kwa ujumla.
Alipoulizwa kwanini
kaamua kujitokeza katika kipindi hiki wakati alipokuwa anajiondoa katika nafasi
ya uenyekiti wa chama hicho alisema kuwa hatojihusisha katika siasa amesema
kuwa amekuwa akiombwa na wanachama na watanzania kutoa ushauri katika
sintofahamu hiyo ya uchaguzi hivyo alichokifanya ni kutoa ushauri akiwa kama
mtanzania wa kawaida na sio vinginevyo.
No comments:
Post a Comment