Wednesday, December 2, 2015

Je Unafahamu kuwa Makondacta wanawake wa magari ya UDA,wengi ni Wake Na Dada wa Madereva --Soma Hii

Na Exaud Mtei

Usafiri Dar es salaam Maarufu kama usafiri wa UDA umekuwa ukiaminiwa na watanzania waliowengi hasa wanaolengwa sana ambao ni wakazi wa Jiji La Dar es salaam kwa kuwa ndio usafiri unaotumiwa na wakazi wengi Wa Jiji hilo kwa sasa na kufanya usafiri huo kuendelea kujichuklulia umaarufu kutokana na uendeshaji wa kazi zake katika Jiji Hilo ambalo linakadiriwa kuwa na wakazi wengi kuliko kajiji Yote Nchini Tanzania.

Mbali na usafiri huo kuwanufaisha wakazi wa Jiji Hili kwa kupata usafiri kwa urahisi na kufanya shighuli zao lakini pia umewanufaisha wakazi wemngi wa Jiji Hili na Tanzania kwa ujumla kupata ajira katika kampuni hiyo pekee ambayo ni mahususi kwa ajili ya kutoa usafiri wa Uhakika katika jiji Dar es salaam ambapo wakazi wengi wamenufaika kwa kupata ajira wakiwemo madereva wa mabasi hayo pamoja na makondakta ambao kwa namna nyingine ni wasaidizi wa madereva katika mabasi hayo.


Moja ya mambo makubwa yanayowavutia wengi katika mgawanyo wa ajira katika kampuni hiyo na ,mabasi hayo ni namna usawa katika jinsia umekuwa ukizingatiwa ambapo ni ukweli usipingika kuwa mabasi ya UDA ndio Mabasi ambayo yamekuwa yakiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi wanawake hasa katika nafasi ya Ukondakta jambo ambalo kwa Tanzania na dunia ya sasa ni jambo geni kutokana na mfumo uliokuwepo kwa kazi kama hizo zilikuwa ni kazi za wanaume na wanawake walikuwa wakionekana kuwa hawana uwezo wa kuhimili kishindo cha kazi na majukumu hayo.

Baada ya mwandishi wa makala hii kugundua swala hilo ili kutaka kujua ni nini kinafanyika hadi kampuni hiyo kuonekana ikiwa na wanawake pamoja nankinadada idadi kubwa kuliko kwa kampuni nyingine zinazotoa aina ya usafiri kama huo Jijini Dar es salaam makala hii inaamua kujikita kufanya mazungumzo na moja kati ya wahusika wa kamouni hiyo ili aweze kutoeleza mfumo mzima wa utoaji ajira katika kampuni hiyo.

Makala hii inafanikiwa kumpata NYAMBI K.NYAMBI ambaye ni afisa masoko wa kampuni Ya UDA ambaye anaanza kwa kueleza kuwa,utoaji wa ajira katika kamouni ya UDA umekuwa ukibadilika badiika kutokana na changamoto mbalimbali ambazo wamekuwa wakikumbana nazo katika swala hili hivyo wamekuwa wakubadilisha mfumo wa upataji waajiriwa kwa muda ili kupata njia sahihi ya kupata watu hao pasipo kuwa na matatizo madogo madogo.

Anaeleza kuwa awali kampuni hiyo ilipoanza ilikuwa inatioa ajira kwa watu watu wote ikiwa na maana ya Dereva na Utingo wake (kondacta) mfumo ambao ulidumu kwa muda mchache kutokana na changamoto kadhaa ambazo walikuwa wanakumbana nazo.

Moja kati ya changamoto ambazo Bwana NYAMBI alizitaja ni kuwa walikuwa wakipokea malalamiko makubwa sana kutoka kwa madereva wao kulalamika kuhujumiwa na makondacta wao kuwa kuwa tunajua mtu anayehusika na swala la hela katika Gari ni Utingo ahivyo malalamiko yakawafikia mengi kama hayo juu ya hujuma za Mkondacta na hata wakati mwingine madereva kulalamikiwa na makondakita kwa changamoto kama hizo.

Hiyo ndiyo iliyowafanya wamiliki wa UDA kubadilisha mfumo mzima wa utoaji wa ajira kutoka kuajiri watu wawili na kuanza kumuajiti dereva pekee ambapo sasa Dereva alitakiwa yeye atafute mtu ambaye anamuamini ili mwisho wa siku yale malamiko yaliyokuwa yanareportiwa huko awali yasijirusie tena.
Kutokana na utaratibu huo mpya wa UDA kumuajiri Dereva Na dereva sasa kuwa na jukumu la kutafuta msaidizi wake yani Utingo (kondacta) Bwana YAMBI Aanasema hapo ndipi idadi kuwa ya madereva wengi waliamua kuwaajiri ndugu zao ambao na kuamua kufanya nao kazi jambo ambalo anasema halikupingwa na liliungwa mkono na kampuni kutokana na kuwa ndio imani ya madereva kuwa zile changamoto za awali zitapungua.

Anasema kuwa idadi kuwa ya wanawake na wadada ambao tumekuwa tukiwaona wakifanya kazi katika magari yao hususani katika nafasi za Utingo asilimia kuwa ni wake wa pamoja na dada wa madereva wa mabasi hayo ambao wameamua kuwaajiri na kufanya nao kazi kutokana na kuwaamini kwa kiasi kikubwa.

Baada ya mfumo huo kuanza kufanya kazi na kwa muda mrefu kidogo sasa Afisa masoko huyo amekiri kwamba kumakuwa hakuna malalamiko sasa ya kutoka kwa madereva wao wa mabasi hayo wala kutoka kwa wasaidizi wao huku changamoto za kuhujumiana baina ya watu hao wawili kwa zikiwa zimepungua kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na hapo awali ilivyokuwa.

Aidha afisa huyo anasema kuwa kuwepo kwa idadi kubwa ya watu wa jinsia ya wanawaake katika kampuni hiyo ni moja kati ya mambo ambayo kampuni hiyo inajivunia kwani inaamini kwa wametioa ajira kwa wanawake japo sio moja kwa moja ila kwa kuwatumia madereva na wanawake nao wamenufaika na ajira za magari hayo.

No comments: