Wednesday, December 23, 2015

Video--Waislam watoa Wito wa amani Kuelekea sikukuu

Mmoja kati ya viongozi wakuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la shia Ithnasheriya nchini Tanzania ambaye pia ni kiongozi mkuu wa chuo cha kiislam cha Imam swadiq Shekh HEMED JALALA akizngumza na wanahabari  mapema leo wakati akitoa salam za sikukuu ya Krismas kwa wakristo wa Tanzania na sikukuu ya mwaka mpya
Watanzania pamoja na wakristo nchini Tanzania wametakiwa kuhakikisha kuwa wanaweka mbele na kuzingatia amani ya Tanzania katika kipindi hiki cha sikukuu za krimas na mwaka mpya kwani amani ya tannzania ndio msingi mkuu wa kuendelea kuijenga nchi yetu.

Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es salaam na mmoja kati ya viongozi wakuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la shia Ithnasheriya nchini Tanzania ambaye pia ni kiongozi mkuu wa chuo cha kiislam cha Imam swadiq Shekh HEMED JALALA wakati akitoa salamu za Krismas kwa wakristo wote nchini pamoja na mwaka mpya kutoka kwa waislam hao  mbele ya wanahabari Jijini Dar es salaam.

Akitoa salamu hizo za Krismas kwa wakristo Shekh JALALA amesema kuwa wao kama waislam wanaamini kuwa wakristo ni ndugu zao kwa misingi ya ubinadamu,ambapo amesema pia undugu huo umejijenga zaidi kijamii na kitaifa hivyo ni jambo muhimu sana kutakiana kheri kwani sikukuu hiyo ni watanzania wote bila kujali itikadi za kidini zilizopo.

Ameongeza kuwa wao kama viongozi wa dini za kiislam wanaamini kuwa kukaa kwa pamoja,kujuana,na kufanyiana wema ni msingi mkuu wa kuhakikisha kuwa jamii inashikamana,inasikilizana,na inajijengea uwezo mkubwa wa kutatua changamoto zao hasa za uvunjifu wa amani kwa jina la dini na itikadi ambapo amewasihi watanzania kuhakikisha kuwa wanailinda amani ya Tanzania katika kipindi hiki cha sikukuu.


Salamu hizo za sikukuu kutoka kwa waislam hao pia zimeambatana na zawadi mbalimbali zikiwemo kadi na zawadi nyingine kwa baadhi ya makanisa ikiwa ni njia ya kudumisha undugu uliopo baina ya dini hizo mbili.  

No comments: