Friday, December 4, 2015

Watumiaji wa simu na Krismasi ya aina yake

Na Mwandishi Wetu

Kwa mara nyingine tena na kama ada ya kila mwaka katika kipindi hiki, sikukuu ya Krismasi inakaribia. Kama yalivyo mazoea  mihemko na kelele za kadi za sikukuu yatakuwapo ila tofauti na zamani, barua, kadi za sherehe za Krismasi n.k sio tena jambo lakujivunia. Wakati jamii ikiwa inafikiria kuhusu hadhi yake  kiuchumi na kijamii kutokana na kukabiliwa na mabadiliko,  hadhi ya mtu binafsi pia imekuwa inaangaliwa. Hivyo ndivyo vipaumbele.
 
Kwa baadhi ya watanzania hivi sasa  licha ya mahitaji muhimu ya binadamu ambayo ni  chakula, malazi, mavazi,  huduma za afya  na elimu  kipaumbele kinachofuata ni kuwa na simu ya mkononi. Hali hiyo inatokana na sababu  njia za mawasiliano zilizozoeleka kama barua  simu za kawaida za nyaya zimeanza kutoweka kwa kasi.  
 
Hata hivyo baadhi ya vitu havitabadilika  inawezekana kusema hivyo  angalau kwa muda mfupi ujao. ‘Makazi asilia’ kwa kuzingatia  mazingira ya kiafrika  siku zote yatabakia kuwa hivyo na ndio maana watanzania wengi wanaoishi mjini nyakati za sikukuu husafiri kuelekea majumbani mwao kwa ajili ya kusherehekea tukio hili la mwaka na wapendwa wao na marafiki wakiwa wamewachukulia zawadi.
 
Kwa hiyo  kufanya manunuzi ya zawadi kwa ajili ya ndugu kunaweza kuwa shughuli  ngumu, lakini hilo halimaanishi kuwa kuibuka na wazo la kufikiria  zawadi ni jambo  lililoepukikika  kutoa zawadi kwa kila  mtu bila kujali jinsia  zao au umri.
 
Watu wanatafuta mbali na kwa mapana, wakijaribu, wakionja  na kutafuta aina  ya zawadi za Krismasi kwa ajili yao  na wapendwa wao  ikiwa ni kuwapatia zawadi nzuri  na ya kipekee.
 
Kwenye enzi hizi za kidijitali  njia mbadala ni nyingi kwa wale wanaotafuta zawadi itakayodumu kwa muda mrefu kwa wapendwa walio na uelewa wa teknolojia itakuwa vipi  kuwepo kwa ongezeko la mawasiliano ya simu za mkononi  hata kwenye maeneo ya ndani vijijini ambako mwandishi wa makala haya ana bibi yake mzee wa miaka 90 na ana simu ya mkononi!
 
Kwa mujibu wa mamlaka ya usimamizi wa mawasiliano Tanzania(TCRA) hivi sasa watumaiji wa simu za mkononi  wanafikia  milioni 32 ambao ni sawa na asilimia 67 ya idadi ya watu wake milioni 45 na idadi hiyo inaongezeka kwa kasi.
 
Katika hali hiyo zawadi ya Krismasi ikiwa ni simu ya mkononi  inashauriwa  kuwa ni zawadi nzuri ambayo mtu anaweza kununua kwa ajili ya mpendwa wake au ndugu katika msimu huu. Ni zawadi ya thamani hata baada ya aliyetoa atakapokuwa amerudi mjini. Kama simu hiyo ya mkononi itakuwa ni  simu ya kisasa  yaani Smartphone  hiyo itakuwa  ni sifa ya ziada  kwa kifaa hicho.
 
Simu za mkononi zenye ubora wa juu  zikiwa na muda wa ziada  wa maongezi  pamoja na vifaa vya simu ya kisasa (Smartphone) ni chaguo lenye haiba ya zawadi ambalo litaifanya mioyo ya wapokeaji  kudunda kwa kasi wakiwa na furaha. Angalau hicho ndio  mwandishi huyu alikigundua baada ya  kufanya manunuzi kwenye duka la Tigo lililopo Mlimani City hivi karibuni.
 
“Wateja wananunua zawadi za simu haraka kuliko  ilivyozoeleka. Aina zote za simu zinanunuliwa haraka hususan aina ya Tecno. Kama unavyoona  tutalazimika kuleta mzigo mwingine  kwa ajili ya mauzo ya kesho,” anasema Linda  ambaye ni muuzaji kwenye duka la Tigo la Mlimani CityDar es Salaam.
 
Kwa kiasi cha shilingi 99,000 mtu anaweza kupata simu aina ya Tecno Y3+  inayotumia kadi mbili za simu ikiwa na skrini ya kugusa, kamera mbili na kumbukumbua ya GB8  ikiwa pia na MB512 na betri yenye uwezo maradufu  (2800mAh) ofa ambayo inavutia na wengi wanaoishi mjini wanaimudu kwa ajili ya kuchukua zawadi ya kumbukumbu  kwa ndugu  wakati wa msimu wa sikukuu.
 
Hali kadhalika kama ipo fursa ya kifedha  kuna zawadi nyingine kwenye ofa hii. Hizi ni pamoja na Huawei Ascend Y625 ikiwa na muda wa maongezi wa shilingi 10,000, GB 4 za intaneti na muziki wa bure kwa mwezi kwa kiwango cha shilingi 225,000 tu pamoja  na Samsung Galaxy J1 ya  kiwango cha juu kwa kiwango cha 250 ikiwa imeunganishwa jumla na  huduma ya 4GLTE  yenye GB 30 za intaneti.
 
Idadi ya ofa za Tigo inaendelea kwa sababu  ofa inaweza kuwa tamu zaidi  kwa kuwa mtu anaweza kununua ZTE Kiss 3, na kuondokana na na kifaa cha kuhifadhi nishati kwa ajili ya simu.
 
Facebook ya Kiswahili
 
Kutokana na ukweli kuwa Watanzania wengi hutumia Kiswahili kama lugha mama ya mawasiliano, Tigo imeshirikiana na kampuni ya Facebook kutoa zana na nyenzo nyingine katika lugha hiyo. Hili hakika litakuwa ni kitovu cha kuuza  na zawadi iliyofungwa  ndani ya lugha ambayo wengi wanaielewa, ikiwa ni zawadi sahihi  hususani kwa wale ambao wanahitaji uelewa wa lugha ya Kiingereza.
 
 
Hii ni mara ya kwanza kwamba huduma ya Facebook  inakuwa ya bure na katika lugha  ambayo watu wengi wanaielewa kwenye mtandao wa simu Afrika Mashariki.
 
Ushirikiano  huo unamaanisha  kwamba wateja wa Tigo  wanaweza kwa mara ya kwanza,  kutumia facebook  kwenye simu zao  bila kuingia gharama za data na  kuunganishwa na watumiaji milioni mbili kwenye mitandao ya kijamii na Facebook yenye  watumiaji bilioni 1.2 duniani kote.

No comments: