Sunday, January 31, 2016

Bomoa Bomoa KIWALANI DAR ES SALAAM yamkumba mtanzania huyu,aomba msaada kwa Rais Magufuli

 Mmiliki wa moja ya GODAUNI la vifaa vya ujenzi  KIWALANI Jijini Dar es salaam katika mtaa wa KIGIRIGIRI GODAUNI NUMBER 117, BW. FURAHA SALUM MAWAMBA ameilalamikia TANROAD kubomoa moja ya GODAUNI lake la vifaa vya ujenzi   bila kufuata sheria hivyo kumsababishia hasara ya BILLION MOJA.
Akizungumza na waandishi wa habari hii leo jijini DAR-ES-SALAAM,MAWAMBA amesema anasikitishwa  sana na kitendo hicho walichokifanya Tanroad kwa madai ya mmiliki huyo kujenga godauni hilo mpaka eneo la barabara,ambapo mmiliki huyo amekanusha kuwa sababu hizo sio za kwel,bali wamefanya hivyo kwa makusudi baada ya kukataa kuwapa rushwa


“maofisa hawa wa TANROAD wamekuwa wakinifwatilia mara kwa mara nakuhitaji rushwa lakini sikutishika na sikuwa tayari kwani navyojua eneo langu lipo mbali na barabara hivyo leo wamebomoa sehemu ya Godown langu na baadhi ya vifaa vyta ujenzi”.amesema mmiliki huyo.

Pia amesema kuwa maofisa hao wa TANROAD hawakupita katika ngazi zinazohusika ikiwemo kwa vongozi wa serikali za mtaa huo kwa mjumbe wala kwa diwani wa eneo hilo hivyo amemuomba Rais Magufuli kuweza kumsaidia kupata haki yake kwani anaamini Rais ni msikivu na mtetezi wa wanyonge.
Mmiliki wa moja ya GODAUNI la vifaa vya ujenzi  KIWALANI Jijini Dar es salaam katika mtaa wa KIGIRIGIRI GODAUNI NUMBER 117, BW. FURAHA SALUM MAWAMBA akiwaonyesha wanahabari baadhi ya nyaraka zinazompa uhalali wa kuwa katika eneo hilo lililobomolewa na TANROAD 
Akizungumza Diwani wa kata ya Kiwalani MUSA KAFANA amesema kuwa kwa sasa anakusanya matatizo ya wananchi waliobomolewa kwa mmoja mmoja na ujumla kuyapeleka kwenye vyombo vya sheria ili Kushughulikiwa kwa wakati huku diwani huyo akikiri kutofwatwa na maofisa kwa ajili ya zoezi la ubomoaji na kusema zoezi hili la ubomoaji ni Batili na uonevu kwa wananchi.

Aidha mmoja wa wananchi katika eneo hilo Mzee HERRY NDELELE amesema kuwa serikali siku zote inapokuja kubomo huwa inatoa taarifa kwa mmiliki wa jengo na uongozi wa mtaa hivyo anashangaa kuona zoezi hilo likifanyika bila utaratibu huo huku akisisitiza serikali kumsaidia mmiliki wa GODAUNI hilo na kumpa haki yake kwani sehemu aliyojenga ni halali na yupo nje ya barabara

“Mimi ni mtu wa zamani sana katika mtaa huu nachojua barabara hii imefuata wananchi na nashangaa kuona kitendo hiki cha kubomolea wananchi kiholela na buila kutowapa stahiki zinazofanana na aamani ya mali zao”amessisitiza

STORY PICHA NA IZACK MAGESA-DAR ES SALAAM

No comments: