Tuesday, January 5, 2016

Mbunge wa Temeke ABDALA MTOLEA afanya ziara Jimboni kwake kukagua hali ya wananchi wake

Mbunge wa Temeke  mh.ABDALA MTOLEA akiwa katika ziara katika Jimbo lake leo kutizama changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa jimbo lake 
 Mbunge wa Temeke  mh.ABDALA MTOLEA,amefanya ziara katika jimbo lake ili kujua changamoto zinazo wakabili wananchi wajimbo hilo.Akizungumza hii leo MH.MTOREA, na wanachi katika kata ya CHANG'OMBE,Huku wananchi wakitoa kero zao mbalimbali.
Swala kubwa likiwemo uvaminzi wamaeneo ya wazikiwemo watu  kuvamia  maeneo  hayo na kuyafanya makazi,wengine kuchukua na kuweka viwanda,tatizo la huduma mbovu ya afya,na uchafu katika mifereji ya maji machafu,mh.MTOREA,amesema atashugurikia kero hizo atajitahid kwa uwezo wake wote kutatua kero hizo kwa wakati huku ukizingatia sasa serikali ni sikivu hivyo amewataka wananchi hao  kuwa na subira.   
Akizungumza mmoja wa wananchi wa kata hiyo ya changombe,HARIMA MATOGORO amesema wanapata shida sana kwa kuvamiwa maeneo mengi ya wazi  katika kata hiyo ikiwemo eneo lililopo tololi changombe kuuzwa na mmiliki wa eneo hilo kuweka kiwanda cha fenicha ambaye mmiliki wake ni OIL COM ,ambacho hutiririsha maji machafu nje ya makazi ya watu.

Pia hakuishia hapo amelalamikia huduma ya afya katika  zahanati ya kata hiyo kuwa ni mbaya,ikiwemo miundo mbinu ya   kutorizisha ,vilevile ukosefu wa dawa,na wauguzi  kuchelewa kuingia ofisini ambapo wanaingia saa tatu na kutoka saa nane,ivyo amemtaka mbunge   kufanyia kazi kero zao hizo   
Pia mtolea amewataka wananchi kushirikiana nae bila kujal itikadi za vyama vyao vilevile amewataka wananchi kuchukia uchafu kutoka moyoni kwan ndicho chanzo cha magonjwa mbalimbali ya mlipuko,ikiwemo kipindupindu,ivyokuwataka wasafishe mazingira yao kuwa safi wakat wote

Baadhi ya changamoto ya mitaro ya maji machafu aliyojionea mbunge huyo
Aidha,diwani wa kata hiyo mh.BENARD NDALUCHAKO  amewataka wananchi kubadilika na kutoa ushirikiano kwa viongozi, ikiwemo kuhuzuria katika vikao vya kata na mtaa bila kujali itikadi za vyama kwani bila wananchi kuonesha ushirikiano kwao   hawawezi kufika mbali na kutekeleza ahadi  hizo kwa usahii ivyo,ushirikiano wa wananchi ni muhimu kwao

No comments: