Wednesday, January 13, 2016

PICHA na VIDEO--ACT wazalendo wazoa wanachama zaidi ya kumi kutoka NCCR,TLP.na UPDP

Naibu katibu mkuu wa chama cha ACT WAZALENDO Ndugu MSAFIRI MTALEMWA akimkabidhi kadi ya uanachama mpya Bi GETRUDA PWIRA aliyekuwa katibu mkuu wa wanawake wa chama cha NCCR mageuzi ambaye pia alishiriki na chama hicho katika harakati zote za uchaguzi mkuu wa mwaka jana,na sasa amejiunga Rasmi na chama cha ACT WAZALENDO chini ya kiongozi mkuu ZITTO KABWE na Mwenyekiti ANNA MGWIRA
NEEMA MSUKWA ambaye alikuwa mwanachama wa chama cha NCCR mageuzi akikabidhiwa kadi mpya ya ACT WAZALENDO
Rukia Mwene Kutoka UPDP naye ni mmoja kati ya wanachama waliotimkia ACT WAZALENDO
 Chama cha ACT wazalendo kiimepokea wanachama zaidi ya kumi (10) kutoka vyama vya TLP,na NCCR-Mageuzi ambao wengi walikuwa ni viongozi wa ngazi mbalimbali ndani ya vyama hivyo pamoja na wanachama wa kawaida.

Baadhi ya viongozi waliojiunga na ACT wazalendo leo ni pamoja na aliyekuwa katibu mkuu wa wanawake NCCR-mageuzi GETRUDA PWIRA, aliyekuwa kiongozi wa vijana wa MUSEVERO KUSAGA pamoja na NEEMA MSUKWA kutoka NCCR,na wanachama wengine wengi.

GETRUDE PWIRA ambaye ametoka NCCR na kujiunga na ACT wazalendo amesema kuwa ameamua kuachana na siasa za uwongo na uzishi na sasa ameamua kuyafwata mabadiliko ya kweli ambayo amedai yapo ndani ya chama hicho chake kipya.

Nimekuwekea video yote ya maelezo ya wanachama hao wapya wa act wazalendo


No comments: