Friday, January 29, 2016

Sakata la Bunge kurushwa TBC LIVE lawaibua LHRC,watoa Tamko kali,Soma Hii

Kaimu mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki zaBinadamu LHRC IMELDA LULU URIO akizngumza na wanahabari mapema leo Jijini Dar es salaam kuhusu sakata lililoibuka  bungeni la TBC kusitisha matangazo ya bunge kwa sababu ya Gharama 
 Na Exaud mtei( Msaka Habari)
Sakata la bunge la Tanzania kutokurushwa moja kwa moja na shirika la habari Tanzania TBC limechukua sura mpya baada ya kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kuibuka na kulaaani maamuzi hayo huku ikiyaita ni kuminywa kwa democrasia na uhuru wa habari nchini Tanzania na kuitaka serikali kuheshimu na kuzingatia mikataba mbalimbali ya kimataifa inayojenga uhuru wa kujieleza kwa nchi wananchama.

Akizungumza na wanahabari mapema leo kaimu mkurugenzi wa kituo hicho IMELDA LULU URIO amesema kuwa kusitishwa kwa matangazo ya bunge na chombo ambacho ni cha umma ni kuonyesha dhahiri kuwa serikali haina nia ya dhati ya kuheshimu yaki ya kupata habari ya kikatiba.

Amesema kuwa sababu zilizotolewa na waziri mwenye dhamana ya habari,utamaduni,sanaa na michezo Mh NAPE NAUYE kuwa kusitishwa kwa matangazo hayo kunalenga kupunguza gharama za uendeshaji ni sababu ambazo zinaleta maswali kuwa gharama hizi ni za nini?,na kwa ajili ya nini?na zikitumika ni kwa manufaa ya nani?,na mchangiaji wa gharama hizi ni nani?huku akisema kuwa TBC ni chombo cha Umma hivyo kunawajibika kwa wananchi wote bila kujali gharama.
Wakili Anna Henga kutoka katika kituo cha sheria na haki za binadamu akizungumza na waandishi wa habari mapema leo ambapo amesema kuwa hakukuwa na sababu yoyote ya kufanya maamuzi hayo kwani kupata habari ni haki ya kila mtanzania 
Ameongeza kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zimesaini makubaliano mbalimbali ya kimataifa inayohakikisha upatikanaji wa taarifa  ikiwa ni pamoja na ule wa OPG –Open government partnership ambao ni jukwaa la serikali zenye uwazi mkataba ambao una misingi ya uwepo wa uwazi,ushiriki,wa wananchi,uwajibikajina uweledi na ubunifu wa kutumia Tehama.
Waandishi wa Habari wakipata Habari
Amesema kuwa LHRC inaitaka serikali kutekeleza kwa vitendo maazimio ya makubaliano ya kimataifa na kikanda katika kulinda haki ya kupata habari na kufuta sheria kandamizi zenye kuminya uhuru huu kwa mfano sheria ya magazeti na sheria ya makosa ya mitandao na kutunga sheria wezeshi.


Pia LHRC wameitaka serikali kuacha kuminya haki za watanzania ya kupata habari za bunge kwa kisingizio cha gharama,na kutenga rasilimalin nyingi kuwezesha shirika hilo waweze kuonyesha moja kwa moja matangazo ya bunge.
Tangazo la kutokuonyeshwa kwa bunge kupitia TBC lilitolewa bungeni na waziri wa Habari NAPE NAUYE na baadae jana waziri mkuu Mh KHASIM MAJALIWA alitoa msisitizo kuwa wameamua kusitisha matangazo hayo kutokana na kupunguza gharama za uendeshaji

No comments: