Mbunge wa Jimbo la Mikumi
ambaye pia ni mwanamuziki wa Hip Hop Tanzania, Joseph ‘Prof Jay’ Haule, ametoa
msaada wa chakula kwa wananchi waliokumbwa na hadha ya mafuriko kata ya Tindiga
jimboni humo.
Katika mafuriko hayo, nyumba
zaidi ya 600 zimeharibiwa na watu zaidi ya 5060 wameathirika na mafuriko
hayo.
Kupitia ukurasa wake wa
Facebook, ameweka bayana kuwa ametoa tani 1 ya unga, maji lita 13000,
Maharagwe, mafuta na dawa za mbu.
“Ndugu zetu wa kata ya
Tindiga wamepata maafa ya mafuriko makubwa sana na mpaka sasa nyumba 600
zimeanguka, kaya zaidi ya 1300 zimeathirika sana na watu 5060 wanahitaji
hifadhi,
Mimi kama mbunge nimepeleka tani moja ya unga, maji lita 13,000, Maharage,
Mafuta ya kupikia, chumvi na dawa za mbu nk
Bado ndugu zetu wanahitaji sana msaada zaidi ili waweze Kukabiliana na hali
ngumu wanayokutana nayo…
Mahitaji ni Maji, Chakula, Mahema, chandarua na dawa za mbu nk
MUNGU AWABARIKI SANA!!!!” ameandika.
|
|
No comments:
Post a Comment