OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA TAARIFA YA MFUMUKO WA BEI LEO

E1
Mkurugenzi wa Sensa za Jamii na Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephrahim Kwesigabo akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira Bi. Ruth Minja.(Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo)
E2
Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Ruth Minja akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei mapema hii leo jjijjini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi wa Sensa za Jamii na Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephrahim Kwesigabo.
E3
Mkurugenzi wa Sensa za Jamii na Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephrahim Kwesigabo akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa beimapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira Bi. Ruth Minja.

………………………………………………………………………………………………
Na; Frank Shija, MAELEZO
Matumizi ya kaya kwenye biadhaa za vyakula imepungua hadi asilimia 38.5 mwaka 2011/12 kutoka asilimia 47.8 ya mwaka 2007.ambapo kwa ujumla wake mfumuko wa Bei umepungu
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Takwimu za jamii na Sensa ya Watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Ephraim Kwesigabo alipokuwa akizunguza na waandishi wa habari kuhusu mfumuko wa bei leo jijini Dar es Salaam.
Kwesigabo alisema kuwa kutokana na mwenendo huo kunaashiria kupungua kwa umasikini wa kipato kwenye kaya kwa kuelekeza matumizi mengine bidhaa zisizo za vyakula kama usafiri, mawasiliano, makazi, maji na nishati.
“Matokeo yanaonyesha kwamba mizania ya matumizi ya kaya kwenye bidhaa za vyakula imepungua hadi asilimia 38.5 mwaka 2011/12 kutoka asilimia 47.8 mwaka 2007” Alisema Kwesigabo.
Aliongeza kuwa makundi mengi mengine yaliyoonyesha kuwa na mizania mikubwa ya matumizi ya kaya mwaka 2011/12 kuwa ni pamoja na Usafi asilimia 12.5 kutoka asilimia 9.5 mwaka 2007, Makazi Maji na Nishati asilimia 11.6 kutoka asilimia 9.2 mwaka 2007 na Mavazi na Viatu asilimia 8.3 kutoka asilimia 6.7 mwaka 2007.
Aidha kumekuwa na ongezeko la Zaidi ya mara mbili ya matumizi ya kaya kwenye kundi la Mawasiliano asilimia 5.6 ikilinganishwa na asilimia 2.1 ya mwaka 2007
Kwa upande wake Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bibi. Ruth Minja amevitaja baadhi ya vigezo muhimu vinavyotumika kupata Fahirisi za Bei zinzoonyesha uhalisia wa matumizi ya kaya binafsi kuwa ni pamoja na mizania katikia bidhaa na huduma muhimu ikiwemo Vyakula, afya, Usafiri ,Maji na Nishati.
Aliongeza kuwa ili kupata matokeo ya mfumuko wa Bei kumekuwa na mtindo wa kufanya marejeo baada ya kila miaka mitano ambapo marejeo ya mwisho yalifanyika mwaka 2007 na kuonyesha matumizi makubwa ya kaya yalikuwa kwenye bidhaa za vyakula zikiwa na asilimia 47.8 ya matumizi yote yakifuatiwa na usafiri asilimia 9.5 huku matumizi madogo zaidi yalikuwa ni huduma za afya kwa asilimia 0.9.
Takwimu hizi zimekuwa zikitolewa kwa mujibu wa sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 na zimekuwa zikisaidia katika kupima na kuboresha sera za kifedha na mipango ya kiuchumi ya kuthibiti mfumuko wa bei, kukadiria pato la Taifa,kuboresha mishahara ya wafanyakazi na mafao ya wafanyakazi waliostaafu.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.