MWIGULU NCHEMBA APASUA JIPU HUKO MIKUMI,AANZA ZIARA NCHI NZIMA KUFUFUA VITUO VYA UTAFITI NA UZALISHAJI MBEGUWaziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akipewa maelekezo na mtafiti wa mbegu kutoka mmoja ya maafisa wa juu wa wakala mkuu wa aghala la mbegu za ASA(Agricultural Seed Agency) Mkoani Morogoro.
Mh.Mwigulu Nchemba akikagua mbegu zilizopo kwenye ghala la ASA mkoani morogoro.
Mwigulu Nchemba akizungumza na watumishi wa ASA(Agricultural Seeds Agency) wakati wa ziara hiyo,Kubwa alilosisitiza ni uzalendo na kufanya kazi kwa kujituma.
Mh.Mwigulu Nchemba akipewa maelekezo kuhusu malisho ya ng’ombe yanayopatikana kwenye kituo cha utafiti wa mifugo -Morogoro(LITA).
Mh:Waziri akiangalia baadhi ya ndama wa Ng”ombe waliopo kwenye shamba la Utafiti kwenye kituo cha LITA-Morogoro
.
Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na Makamu Mkuu wa chuo za SUA(Sokoine University of Agriculture) alipofika kwaajili ya kukutana na wataalam,na uongozi wa SUA kwaajili ya kupokea maoni yao kuelekea kilimo,ufugaji na uvuvi wa kisasa. “Transformation of Agriculture”.
Katika kikao hicho,Wataalam kutoka SUA walisisitiza kuwa ili Tanzania iweze kuondokana na kilimo holela,ni wakati muafaka sasa kama nchi kuamua kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji na kuondoakana na kilimo cha mvua,pia kuachana na jembe la mkono na wakati huo huo kuimarisha vituo vya utafiti na kuzalisha mbegu kikanda.
Akiwa njiani kuelekea Ifakara,Mwigulu Nchemba anaamua kufanya mkutao Jimbo la Mikumi kijiji cha Tungu kwaajiliya kusikiliza kero za wananchi dhidi ya uongozi wa miwa wilaya,Mkoa na Taifa,mahusiano mabaya ya kibiashara kati ya wakulima wa miwana kiwanda cha ilovo,Lakini utitiri wa vyama vya wakulima kwa eneo lakilombero.
Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mbunge wa Mikumi Mh.Joseph Haule(Prof.Jay) wakati wa mkutano huo
Baada ya kusikiliza kero kutoka kwa wananchi na kusoma baadhi ya ripoti za serikali ya wilaya na mkoa na zile za Tume mbalimbali zilizounda kujua kiini cha matatizo ya wakulima wa miwa-Kilombero,Mwigulu Nchemba akiwa ndiye waziri mwenye dhamana na kilimoa akaamua kufuta uongozi wote kwa wakulima wa miwa kuanzia ngazi ya wilaya ya Mikumi hadi Taifa kwa kosa la ubadhilifu na matumizi mabaya ya madaraka.
Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia mfereji ulioandaliwa kwaajili ya kusambaza maji kwenye shamba la utafiti wa mbegu za Mpunga-Kilombero.Matumizi ya mifereji kwenye kilimo yanaondoa mfumo wa kutegemea mvua ilimimea kupata maji na kukua kwa wakati.
Mwigulu Nchemba anatarajia kuendelea na ziara ya kukagua vituo vya Utafiti na uzalishaji wa mbegu nchi nzima,lakini wakati huo huo atatembelea mashamba ya mifugo na maeneo ya uvuvi wa samaki.
Picha/maelezo na festo Sanga Jr

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.