Friday, March 4, 2016

TAARIFA RASMI KUHUSU HABARI ZA KUTENGWA KWA ZITTO KABWE ACT ZANZIBAR


TAMKO LA CHAMA KUHUSU ACT PEMBA WAMTENGA ZITTO KABWE


Chama cha ACT Wazalendo kimesikitishwa na na kinalaani taarifa ilichapiswa na iliyosambazwa leo tarehe 03 Machi, 2016  na Gazeti la Raia Tanzania kwamba wanachama watano (5) na waliokuwa wagombea wa uwakilishi kwa tiketi ACT Wazalendo Pemba wakimuhusisha Kiongozi wa Chama ndugu Zitto Zubeir Kambwe kwamba amefuata msimamo wa CUF katika kufikia uamuzi wa kutoshiriki Uchaguzi wa marudio Zanzibar tarehe 20 machi, 2016.


Jambo hili si  kweli kwani msimamo wa kutoshiriki umefanywa na vikao vya Kamati Maalum ya Zanzibar tarehe 05 Februari, 2016 na Kamati Kuu ya Chama tarehe 13 Februari,2016.

Chama hakikutegemea kwamba wanachama na viongozi makini wangeweza kumuhusisha binafsi Kiongozi wa Chama na kulifanya suala hili kuwa la kibinafsi na wakitambua kuwa ni maamuzi ya vikao halali kwa mujibu wa Katiba.

Aidha katika taarifa yao wamesema kuwa ACT Wazalendo haikuwa na sababu kususia uchaguzi wa marudio jambo ambalo pengine wao ingefaa wakaeleza pia faida za kushiriki uchaguzi wa marudio ambao waangalizi wote wa ndani na nje ya nchi wamethibitisha kuwa hawatoshiriki kwa sababu uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba, 2015 ulikuwa huru na wa haki
Kukihusisha Chama na msimamo wa CUF na UKAWA ni mawazo potofu na mgando. Uchaguzi wa Okotoba 25,2015 ulihusisha vyama 14 na wakati ule hawakusema kama tunaunga mkono CUF au UKAWA inakuwaje baada ya Uchaguzi kufutwa katika mazingira ya utatanishi kwambwa Chama makini kishindwe kutoa maamuzi makini.

ACT Wazalendo haijawahi na  haitawahi fuata misimamo ya vyama vyengine kwa sababu ina viongozi wanaojiamini katika kufanya maamuzi yenye manufaa kwa taasisi. Ambao hawajiamni hawana nafasi ya kuingiza migogoro ndani ya chama.

Aidha miongoni mwa wanachama hao watano 5 hakuna hata mmoja ambae ni mjumbe wa vikao vya chama na inaonekana wametawaliwa na tamaa ya fisi na maslahi binafsi zaidi ya masilahi ya Chama, Taifa na misingi ya demokrasia.

Chama cha ACT Wazalendo kinaendelea kusisitiza kuwa hakikubaliani kwa vyovyote vile na  suala la kufutwa kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2016 na kuitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar  ZEC ikamilishe mchakato wa kujumlisha na kuhakiki matokeo ya urais yaliyokuwa yakiendelea vizuri hadi kutangazwa kwa majimbo 31 na hatimae mshindi  HALALI atangazwe ili nchi ipate viongozi halali kwa utaratibu wa kidemokrasia tuliojiwekea.

Mwisho ACT Wazalendo inaendelea kusisitiza kuwa haitashiriki uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 machi, 2016 na kwamba mwanachama au kiongozi yoyote anayepingana na maamuzi ya Chama atakuwa amejivua mwenyewe uanachama na kwa waliokuwa wagombea kwa tiketi ya ACT Wazalendo watambue kwamba si wagombea tena wa Chama na kwamba wasitumie jina la Chama bali wasimame kama wagombea binafsi.

Chama cha ACT Wazalendo hakitapokea taarifa wala matokeo yoyote yatakayotangazwa na ZEC katika uchaguzi wa Marudio na kwamba matokeo hayo yatakuwa yao binafsi kwa masilahi binafsi.

Pamoja na salaam za chama.
Taifa kwanza leo na kesho.

Juma Said Snani
Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
Zanzibar 
  

No comments: