Monday, March 21, 2016

Wilaya ya Newala na Tandahimba mkoani Mtwara zimetenga fedha za mapato ya ndani ili kukabiliana na uhaba wa madawati pamoja na madarasa.


Mtwara.

Wilaya ya Newala na Tandahimba mkoani Mtwara  zimetenga fedha za mapato ya ndani ili kukabiliana na uhaba wa madawati pamoja na madarasa.

Hayo yameelezwa na kiongozi wa kamati ya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo mkoa wa Mtwara,Amani Rusake wakati wa ziara ya ukaguzi na kubainisha wilaya ya Tandahimba zaidi ya 150 mil zimetengwa kutoka mapato ya ndani na mfuko wa elimu kwaajili ya elimu ili kutengeneza madawati mapya na kukarabati yaliyoharibika.


Alisema kwa wilaya ya Newala kiasi cha Sh 90 mil zimeombewa kubadilishwa matumizi kwaajili ya utengenezaji wa madawati na wilaya ya Tandahimba ofisi ya mkurugenzi tayari imeunda kamati kwaajili ya kufuatilia miti inayofaa kwaajili ya mbao ili kuomba kibali maliasili.

“Mwitikio mkubwa wa elimu bure umepelekea ongezeko la mahitaji ya madawati na vyumba vya masomo tofauti na ilivyokuwa zamani lakini  halmashauri zetu tayari zina mikakati ya kuhakikisha wanaondoa changamoto iliyopo kabla ya mwezi June ikiwa  ni utengaji wa pesa za mapato ya ndani ,"alisema Rusake
Akizungumza mkuu wa shule ya Mdimba kata ya Mnyoma wilaya ya Tandahimba, Abdallah Majosa alisema kuwa baada ya kutangazwa elimu bure kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wanafunzi kuripoti shuleni kama walivyopangiwa.

“Shule yangu inakabiliwa na uhaba wa madarasa na madawati,kidato cha kwanza wote wanakaa chini,hii imesababishwa na mwitikio mkubwa wa elimu bure kwasababu wote waliopangiwa wameripoti tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyama kwahiyo kumekuwa na ongezeko la madawati na vyumba vya kusomea,”alisema Majosa
Akizungumza mtendaji wa kata ya Mnyoma Said Mtondo alisema kuwa halmashauri tayari imewakata wakulima wa korosho Sh 20 kwa kila kilo wanayouza kwaajili ya mfuko wa elimu.


“Wakulima tayari walishakatwa na halmashauri Sh20 kila kilo kwaajili ya mfuko wa elimu kwahiyo sasa hivi kumwambia tena mzazi achangie ni kitu ambacho kinabidi  kiwe hiari lakini halmashauri tayari kuna mikakati ya kukabiliana na hili ikiwa ni pamoja na kupasua mbao ili madawati yapatikane,”alisema Mtondo

No comments: