HOT--DARAJA LA KIGAMBONI LAMSOMBA MKURUGENZI WA JIJI LA DAR,MAGUFULI AMTUMBUA JUU YA DARAJA


BREAKING NEWS....

Rais Magufuli ame msimamisha kazi mkurugenzi wa jiji (DAR) ndugu Wilson Kabwe kwa tuhuma za ufisadi!
Aidha ikumbukwe kwamba RC Paul Makonda alitoa tuhuma dhidi ya Wilson Kabwe na kuomba Rais amuondoe kwa kukubali na kuidhinisha mikataba yenye harufu ya ufisadi katika mradi wa mabasi yaendayo kasi, na tozo katika stendi ya Ubungo!

Niweke kumbukumbu sawa: Wilson Kabwe aliwahi kuwa Mkurugenzi wa jiji la Mwanza na baadae akatuhimiwa na aliye kuwa mbunge wa jimbo la Nyamagana (Ezekiel Wenje) Kikwete kama ilivyo kuwa kawaida akampeleka Mbeya ambako nako alilalamikiwa na kupelekwa tena DAR!

NB: Miaka michache iliyo pita, jiji la Mwanza lilipata HATI CHAFU kupitia ukaguzi wa CAG! Hapa tunaona Kuna jipu lilikuwa LIKIFUGWA muda mrefu sana.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.