SDL LIGI NDOGO KUANZA MEI 11

FDLKamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuanza kwa ligi ndogo Mei 11, 2016 katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam itakayozishirikisha jumla ya timu nne.
Timu zilishoshika nafasi ya pili katika msimamo wa SDL kwa kila kundi, Abajalo FC (Dar es salaam), Pamba FC (Mwanza), Mvuvumwa (Kigoma), Mighty Elephant (Songea) zitacheza ligi hiyo kusaka timu mbili zitakazoungana na timu nne za juu kupanda ligi daraja la kwanza (FDL) msimu ujao.
Klabu nne za Allicane Schools (Mwanza), Mshikamano FC (Dar es salaam), Mbeya Warriors (Mbeya) na Singida United (Singida) zilizoongoza msimamo wa makundi ya SDL zitaungana na timu mbili kupanda ligi daraja la kwanza msimu ujao.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.