Wadau wakifurahi usiku wa jana wakati wa hafla ya mchapalo baada ya Tigo na mgahawa wa samaki samaki kuingia Ubia ambapo pande hizo mbili zimekubaliana kufanya kazi pamoja kwa kuleta bidhaa/huduma zao kwa wateja wa kila mmoja. |
|
Vinywaji murua kabisa |
|
Warembo wa Tigo wakiwa tayari kuhudumia wateja na wageni waalikwa wote |
|
Ulinzi ukiimarihwa kwa wageni waalikwa na wateja wote |
|
Mtaalamu wa mitandao ya kijamii kutoka Tigo Samira Baamar (kulia ) akiwa katika pozi na wafanyakazi wenzake Ummy Mtiro na Natasha |
|
Mhudumu wa Samaki akitabasamu na kuwakaribisha wageni waalikwa |
|
Blogger na mdau wa mitandao ya kijamii John Kiandika akiwa katika pozi na mkewe wakati wa hafla usiku wa jana |
|
Mmoja ya wageni waalikwa akipata maelezo kuhusu huduma ya Tigo 4g kutoka kwa mhudumu |
|
Mkurugenzi wa migahawa ya Samaki Samaki, Bw. Carlos Bastos |
|
Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo Oliver Prentout akifurahi jambo na wafanyazi wa tigo wakati wa hafla hii |
|
Watangazaji maaruf wa kituo cha Clouds tv Hudson Kamoga na Sam sasali wakiwa pamoja kupata maelekezo kuhusa huduma ya intanet ya kasi ya Tigo 4G kwenye hafla hiyo. |
|
Mhudumu akiandaa chakula |
|
Wahudumu wa samaki samaki wakiwa katika pozi |
|
wadau wakiwa katika pozi |
|
Taswira ukumbini |
|
Mdau John kiandika na mkewe wakipata maelezo zaidi kuhusu huduma ya Tigo 4g |
|
wadau wakiwa kwenye picha ya pamoja |
Tigo ni kampuni ya mawasiliano ya simu za mikononi yenye ubunifu mkubwa nchini Tanzania,ikijulikana kama“nembo ya maisha ya kidijitale yanayojitosheleza”.
………………………………………………………………………………………………………
Inatoa huduma mbalimbali kuanzia huduma ya sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedhaza kwenye mitandao ya simu za mikononi, Tigo imeanzisha ubunifu kama vile Facebook ya Kiswahili, Kiunga cha Tigo Pesa kwa watumiaji wa simu za Android & iOS, Tigo Music ( Deezer)na huduma ya kwanza Afrika Mashariki kutuma fedha kwa njia ya simu za mikononi nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili sarafu ya nchi husika.
Intaneti ya Tigo ya 3G inatoa huduma bora kwa wateja wake katika mikoa yote nchi nzima, na Hivi karibuni Tigo imezindua mtandao wa 4G ambao kwa sasa unapatikana Dar es Salaam nzima, na unatarajiwa kuzindualiwa nchi nzima. Kati ya mwaka 2013 na mwaka 2014 pekee kampuni ilizindua zaidi ya minara mapya 500 yenye mtandao wa Tigo nakufanya kuwa zaidi ya maeneo 2000 ya mtandao na inapanga kuongeza uwekezaji wake mara mbili ifikapo 2017 katika suala la upatikanaji wa mtandao na kuongezauwezo wa upatikanaji wa mtandao kwa maeneo yasiyofikika kabisa vijijini.
Pamoja na kuwa na zaidi ya wateja milioni 10 waliosajiliwa, Tigo imeajiri zaidi ya watanzania 300,000 ikiwa ni pamoja na mtandao wa wawakilishi wa huduma kwawateja, wafanyabiashara wakubwa wa fedha za kwenye simu za mikononi, mawakala wa mauzo na wasambazaji.
Tigo ni nembo kubwa ya kibiashara ya kampuni ya Millicom, kampuni ya kimataifa inayoendeleza maisha ya kidijitale katika nchi 11 pamoja na shughuli za kibiashara katika Afrika na Amerika yaKusini na ina ofisi kubwa Ulaya na Marekani.
Ukiwa ni mgahawa unaoongoza kwa vyakula vinavyotokana na mazao ya baharini na vinywaji nchini Tanzania, Samaki Samaki inamiliki migahawa mitatu ambayo ipo Mlimani City
(Ubungo/Mwenge), City Centre (kwenye makutano ya Barabara ya Samora na Mirambo) na Samaki Samaki kwenye Barabara ya Haile Selassie.
Tangu kuanzishwa kwa tawi la Mlimani City mwaka 2007 tumeshuhudia kupanuka kwa Migahawa ya Samaki Samaki hadi matawi miwili zaidi ndani ya jiji la Dar es Salaam katika kipindi cha miaka mitano ya uendeshaji wake, kuongezeka kwa wateja ambao wanafikia hadi 1,000 kwa siku ndani ya matawi hayo, kuongezeka kuimarika kwa nembo yetu ya biashara na kutambuliwa na umma, kupatikana kwa fursa za ajira kwa wazawa, jamii kutuunga mkono kupitia Mfuko wa Samaki Samaki ( Samaki Samaki Foundation) ambao unalenga kuwasaidia wahitaji kwa kutoa misaada ya kuwajibika kwa jamii, jamii imeweza kutufikia kwa kutumia video na muziki uliorekodiwa katika kukuza nembo yetu kupitia Samaki Samaki Fleva na kuuza bidhaa zetu nyingine ambazo hazihusiani na chakula zikiwemo kofia, fulana na CD za muziki.
Dira ya Samaki Samaki ni kushikilia nafasi yake nchini Tanzania kwa kukua hadi mikoa mingine nchini na hata baadaye kusambaa hadi kona nyingine za Afrika na dunia kwa ujumla. Kwa hivi sasa inaangalia Mwanza na Arusha kama vituo vya kuanzia kusambaa hadi mikoa mingine.
No comments:
Post a Comment