Saturday, April 2, 2016

TUKIO KUBWA SANA DAR ES SALAAM MCHANA HUU,NAIBU WAZIRI WA ELIMU ALIONGOZA

Naibu waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Stella Manyanya akishiriki matembezi ya maadhimisho ya siku ya watu wenye usonji Duniani ambayo imeadhimishwa leo Jijini Dar es salaam
 Na Exaud Mtei (Msaka Habari)
Serikali ya Tanzania imesisitiza kuwa itaendelea kutoa elimu bora na Bure kwa watoto wote wa kitanzania bila kubagua rangi,kabila wala dini huku mkazo mkubwa sasa ukielekezwa pia kwa watoto wenye ulemavu na mahitaji maalum lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa watoto wote wa Tanzania wanapata elimu sawa.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Stella Manyanya  wakati akisoma hotuba ya Makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mama SAMIA SULUHU wakati akimwakilisha katika maadhimisho ya siku ya watu wenye usonji duniani ambayo huazimishwa kila mwaka tarehe mbili ya mwezi wanne.

Akisoma hotuba hiyo Eng Manyanya amesema kuwa serikalI ya awamu ya tano chini ya Rais DR JOHM MAGUFULI imedhamiria na imeamua kutoa elimu bure katika ngazi ya elimu ya msingi pamoja na kupanua fursa ya elimu kwa watoto wenye uhitai maalum kwa kuandaa walimu,kuboresha miundo mbinu na kutoa kipaumbele kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika elimu.

Mhe. Dr. POSSY Abdallah. Naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu Mkuu Sera, kazi, Ajira, Bunge, Vijana na walemavu...akishiriki matembezi hayo leo Jijini Dar es salaam
Aidha katia maadhimisho hayo ambayo yameandaliwa na taasisi ya Khoja Shia Itha Asheri Jamaat na kufanyika katika viwanja vya shule ya AL MUNTAZARI Mh Naibu waziri ameipongeza sana taasisi hiyo kwa kufanikiwa kuwa msatari wa mbele katika kuwahudumia watoto wenye matatizo ya Usonji na mahitaji mengine maalum kwa kuwapatia Elimu kulingana na mahitaji yao,ambapo amewataka wadau mbalimbali wakiwemo Walezo,wazazi na taasisi nyingine kuunga mkono juhudi hizo ili kuwajenga watoto hao waweze kuwa msaada katika taifa la Tanzania.
Usonji ni upungufu wa kibaiologia anaopata mtoto anapokuwa tumboni kwa mama yake na dalili zake huonekana kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea ambapo.

Maadhimisho ya watu wenye usonji huazimishwa kila tarehe 2, ya mwezi april ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa “TUWAPENDE NA TUWALINDE.Picha zaidi Bofya chini








Mhe. Dr. POSSY Abdallah. Naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu Mkuu Sera, kazi, Ajira, Bunge, Vijana na walemavu...


 





No comments: