Watuhumiwa 472 wahukumiwa adhabu ya kifo nchini Tanzania,LHRC wazindua Repoti yao yao ya Haki za Binadamu

Mgewni Rasmi katika uzinduzi huo ambaye ni Jaji mfawidhi wa mahakama ya mwanza Robert Makaramba na Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu nchini LHRC Bi Hellen Kijo Bisimba wakionyesha juu ripoti hizo mara baada ya kuzinduliwa Rasmi leo Jijini Dar es salaam 

Jaji mfawidhi wa mahakama ya mwanza Robert Makaramba akitoa hotuba yake katika hafla hiyo 
Jaji mfawidhi wa mahakama ya mwanza Robert Makaramba akiwakabidhi baadhi ya wageni mbalimbali waliofika katika uzinduzi huo Ripoti hiyo leo Jijini Dar es salaam 
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu nchini LHRC Bi Hellen Kijo Bisimba akizngumza katika hafla hiyo
 Na Exaud Mtei

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC) Kimezindua Ripoti ya hali na mwenendo wa haki za binadamu nchini  ripoti ambayo imebaini kuwa kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo haki ya kuishi.


Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyozinduliwa na Jaji mfawidhi wa mahakama ya mwanza Robert Makaramba imebainisha kuwa mahakama nchini zimekuwa zikiendelea kutoa adhabu ya kifo japo kuwa haki ya kuishi imeanishwa katika katiba ya Jamuhuri wa Muungano ya mwaka 1977.

''Katika mwaka 2015 jumla ya watuhumiwa 472 walihukumiwa adhabu yakifo ambapo ni zaidi ya watu 62 waliohukumiwa katika kipindi cha mwaka 2014 kati ya hao watuhumiwa walihukumiwa adhabu ya kifo wanaume 452 wanawake 20 adhabu ya kifo inakiuka haki yakuishi ''Imeeleza Ripoti hiyo .

Aidha katika ripoti hiyo imeeleza kuwa  maoni kuhusiana na adhabu ya kifo yamekuwa yakigawanyika huku mashambulizi ya watu wenye ulemavu wa ngozi Albino yamekuwa yakisababisha watu wengi kutoa maoni kuhusiana na adhabu hiyo .

Imebainisha kuwa matukio ya kujichukulia sheria mkononi yamekuwa yakiongezeka katika kipindi cha mwaka juzi ikilinganishwa na kipindi cha mwaka jana ambapo matukio 997 yalitokea ikilinganishwa na matukio 785 yaliweza kutokea katika kipindi cha mwaka 2015 .

''Taarifa kutoka kwenye vyombo vya dola vilibainisha kuwa kumekuwa na maongezeko ya vitendo vya mauaji katika mikoa ya simiyu,Dar es salam pamoja na njombe ''Iliongeza Ripoti hiyo .

Ripoti hiyo iliongeza kuwa mbali na kuwepo kwa vitendo vya mauaji katika mikoa hiyo pia ripoti hiyo ilibainisha watu wengi zaidi waliweza kupoteza maisha yao kutokana na ajali za barabarani ikiwemo bodaboda ambapo jumla yawatu 2,626 walipoteza maisha kutokana naajali hizo.
Baadhi ya picha nyingine zipo chini
About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.