Friday, April 8, 2016

ZITTO KUHUDHURIA KOZI YA UONGOZI CHUO KIKUU CHA HAVARD NCHINI MAREKANI


Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Ndugu Zitto Zuberi Kabwe, atakuwa nje ya nchi kuanzia Tarehe 7 Aprili hadi 29 Aprili mwaka huu kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kuhudhuria mkutano wa wabunge  kutoka nchi tofauti  duniani mkutano ulioandaliwa na Benki ya Dunia nchini Marekani.

Kwenye mkutano huo Ndugu Zitto Kabwe atatoa mada kuhusu masuala ya hifadhi ya jamii kwa watu walio kwenye sekta isiyo rasmi. Pia atahudhuria kozi maalum ya uongozi katika Chuo Kikuu cha Harvard, nchini Marekani.


 Kutokana na safari hiyo na kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha ACT-Wazalendo ya mwaka 2015, Ibara ya 29 ibara ndogo ya (25) kipengele cha (xi), Kiongozi wa Chama amemteua Ndugu Yeremia Kulwa Maganja ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Serikali za Mitaa Taifa, kukaimu nafasi ya Kiongozi wa Chama kwa muda ambao hatakuwepo nchini

Kiongozi na Mwenyekiti wa Chama, wanamtakia Ndugu Maganja utekelezaji bora wa majukumu yake kama Kiongozi wa Chama katika kipindi hicho.

Pamoja na Salaamu za Chama, ACT-Wazalendo! Taifa kwanza leo na kesho

 Maingu Samson Mwigamba KATIBU MKUU __

No comments: