DRFA,YAJIVUNIA KLABU ZAKE KUMALIZA MSIMU 2015/2016 KWENYE NAFASI ZA JUU.Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA imezipongeza klabu zake tatu za ligi kuu kwa kumaliza katika nafasi za juu kwenye michuano ya ligi kuu soka tanzania bara.
Timu hizo ni Yanga SC iliyomaliza katika nafasi ya kwanza,Azam FC iliyomaliza katika nafasi ya pili na Simba SC  iliyomaliza katika nafasi ya tatu.
Mwenyekiti wa Drfa,Almas Kasongo amesema mafanikio hayo wanayapeleka moja kwa moja kama zawadi kwa mkuu wa mkoa wa Dar  es salaam Mh .Paul  Makonda,ambaye ameonesha mchango mkubwa kwa kuhimiza watu kupenda michezo.
Amesema kama chama hawana budi kujivunia mafanikio hayo na kuwapongeza wachezaji,walimu na viongozi wa vilabu vyote vitatu kwa hatua hiyo inayozidi kuupamba mkoa wa Dar es salaam kisoka.
 
 MAKUMBUSHO,SIFA POLITAN,ZIMA MOTO ZATAKIWA KILA LA KHERI LIGI ZA MIKOA.
DRFA,inazipongeza timu za Makumbusho FC,Sifa Politan na Zima Moto kwa kufanikiwa kuingia katika ligi za mikoa baada ya kufanya vizuri katika michezo yao.
Klabu ya Zima Moto itakwenda kucheza mkoani Njombe,wakati Makumbusho na Sifa Politan wanakwenda kucheza mkoani Morogoro.

Pia klabu ya Abajalo FC  nayo imepongezwa kwa mafanikio ya kutinga ligi daraja la kwanza,na kuwataka kuzidisha mapambano ili wapige hatua nyingine zaidi ya kufika ligi kuu.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.