Thursday, May 5, 2016

Part 3-CHAMA CHA ADC SASA SAFII HALI YATULIA,MSAJILI AWARUHUSU WAENDELEE BILA MWENYEKITI WALIYEMTIMUA

Naibu katibu mkuu wa ADC Bwana DOYO HASSAN DOYO akisalimiana na moja kati ya wajumbe waliowasili Jijini Dar es salaam kwa ajili ya mkutano huo
Baada ya mgogoror wa muda mrefu wa kiuongozi ndani ya chama cha ALLIANCE FOR DEMOCRATIC FOR CHANGE-ADC hatimaye habari zinasema kuwa msajili wa vyama vya siasa amewaruhusu viongozi waliosalia ndani ya chama hicho kuendelea na shughuli zao za kisiasa ikiwemo mikutano ya kiuongozi ndani ya chama hichochanzi chetu kimeeleza.

Hapo awali msajili wa vyama vya siasa aliawaamuru viongozi wa chama hicho kumrudisha kazini aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho aliyetimuliwa na bodi ya wadhamini ya chama hicho jambo ambalo pia lilishindikana baada ya viongozi hao kumkataa mwenyekiti huyo SAID MIRAAJ kwa madai kuwa wamemtimua kwa mujibu wa katiba ya chama hicho
Wajumbe wa Mkutano mkuu wa chama hicho wakiwasili jijini Dar es salaam toka mikoa mbali mbali baada ya msajili wa vyama vya siasa kutoa ruhusa ya Chama cha ADC kuendelea na vikao vyao vya kikatiba kwamjibu wa katiba ya ADC. Leo Tarehe 5-05-2016 kunatarajia kufanyika kikao cha bodi ya uwongozi taifa na Tarehe 8-05-2016 siku ya jumamosi Kuna tarajiwa kutafanyika Mkutano mkuu taifa wa kuchagua viongozi wa kitaifa.
 





No comments: