Mwenyekiti wa chama cha ALLIANCE FOR DEMOCRATIC FOR CHANGE -ADC chenye maskani yake Buguruni SAID MIRAAJ akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam leo |
Baada
ya jana baadhi ya viongozi mbalimbali wa chama cha ALLIANCE FOR DEMOCRATIC
CHANGE -ADC wakiongozwa na Naibu katibu mkuu wake DOYO HASSAN DOYO kuibuka na
kumtuhumu mwenyekiti wa chama hicho SAID MIRAAJ pamoja na msajili wa vyama vya
siasa kwa kukihujumu chama hicho Hatimaye mwenyekiti huyo ameibuka leo na
kueleza mazIto juu ya mgogoro huo ndani ya chama.Anaandika Exaud Mtei kutoka
Dar es salaam
Akizunguma na
wanahabari leo Jijini Dar es salaam mwenyekiti huyo anayedaiwa kutimuliwa
katika nafasi hiyo amesema kuwa mgogoro ndani ya chama hicho umeletwa na
mwanachama wa kawaida ambaye ni HAMAD RASHID ambaye amesema lengo lake ni
kukitaka kiti hicho cha uenyekiti kinyume na taratibu za chama.
Amesema kuwa tangu
kumalizika kwa uchaguzi wa awali visiwani Zanzibar HAMAD RASHID ambaye alikuwa
mgombea wa chama hicho Visiwani Zanzibar amekuwa akitoa matamko yanayokihusu
chama bila kuwashirikisha viongozi halali wa chama hicho likiwemo tamko la
kukubali kushiriki katika uchaguzi wa marudio wa Zanzibar tamko ambalo amesema
halikuwa na Baraka za chama hicho.
MIRAAJ amewaeleza
wanahabari kuwa yeye kama mwenyekiti wa chama alimpokea HAMAD RASHID kama mwanachama wa kawaida na
baadae kukubali awe mlezi wa chama hicho kutokana na ukongwe wake katika siasa
za Tanzania lakini hawakumpa kazi ya usemaji wa chama kwani kwa mujibu wa
katiba ya chama hicho msemaji pekee wa chama hicho ni mwenyekiti.
Aidha Ameelaza kuwa
kazi pekee ya mlezi wa chama ni kuwashauri viongozi wakuu wa chama na sio kutoa
maamuzi ya chama kama aliyoyafanya ya kukubali kurejea uchaguzi wa Zanzibar bila
ridhaa ya mwenyekiti na vyombo husika vya chama,huku akimtaka aache kuivuruga
katiba ya chama hicho.
Amesema kuwa kwa mujibu
wa katiba ya chama hicho baraza la wadhamini la chama halina nguvu yoyote
kisheria ya kumuondoa mwenyekiti madarakani kamali livyofanya hivyo yeye
ataendelea kuwa mwenyekiti wa chama hicho hadi pale ambapo itaamuliwana na sheria
kuwa hafai kuwa mwenyekiti huku akisema anajipanga kwenda kwa msajili wa vyama
vya siasa hapo kesho kumweleza masikitiko yake ya kuzuiwa na watu ambao
amewaita wahuni ndani ya chama kurejea katika ofisi zake kama kawaida.
Hapo jana Naibu katibu
mkuu wa chama hicho DOYO HASSAN DOYO aliwaeleza wanahabari kuwa mwenyekiti huyo
haruhusiwi kufika katika eneo lolote la ofisi za chama hadi apate mwaliko
maalum wa chama hicho tamko ambalo mwenyekiti huyo SAID MIRAAJ amelikanusha na
kusema kuwa limeandikwa kihuni na wahuni wanaotaka kukivuruga chama na yeye hayupo
tayari kuwavumilia.
Ameongeza kuwa tamko la
chama hicho kwa wanahabari la jana halina uhalali kwa kuwa limeandikwa kihuni
bila saini ya mwandikaji,bila jina la mwandikaji hivyo hakuna tamko la chama
linalotoka hivyo.
Mgogoro ndani ya chama
hicho uliibuka mara tu baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa kwanza wa Zanzibar ambapo
swala la uchaguzi wa marudio liliwagawa viongozi hao huku ikionekana wazi kuwa
mwenyekiti huyo hakuwa tayari chama cha ADC kushiriki katika uchaguzi huo huku
mgombea HAMAD RASHID ambaye ameonekana kuwa na nguvu ndani ya chama hicho
kushiriki katika uchaguzi huo uliopelekea chama cha mapinduzi kuibuka na ushindi
mnono.
No comments:
Post a Comment