Mwenyekiti wa Shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania (TAHAFE), Sheikh Abdallah Khalid (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu mchakato wa kwenda kuhiji mwaka huu 2016. Kushoto ni Katibu wa Taasisi hiyo, Dk. Ahmed Twaha na kulia ni Mjumbe, Hassan Ali.
Katibu wa Shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania (TAHAFE), Sheikh Abdallah Khalid , akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
OFISI Kuu ya Hijja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezitangaza taasisi 31 zilizokidhi vigezo vya kupeleka mahujaji kwenda kuhiji kwa mwaka 2016.
Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania (TAHAFE) Sheikh Abdallah Khalid wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana.
Alisema shughuli zote za utekelezaji wa ibada ya Hijja na Umra hapa nchini zinasimamiwa, kuratibiwa na kuendeshwa chini ya uongozi wa Biita inayoundwa na Shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania (Tahefa) na Umoja wa Taasisi za Hijja Zanzibar (Utahiza).
Alisema gharama za mahuja kwa mwaka huu kutoka nchi kwenda kuhiji ni dola 3400 hadi 4700 na kuwa malipo ya huduma stahili yanapaswa kupitia benki zilizoanishwa na Wizara ya Hijja Saudia Arabia.
Sheikh Khalidi alisema taasisi zote zinatakiwa kuwapima afya mahujaji watarajiwa mapema kuanzia Agosti 8 au kabla ya hapo na kujaza fomu maalumu zitakazotolewa na Biita na kuingizwa kwenye mtandao.
No comments:
Post a Comment