Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akitoa ufafanuzi kuhusu wizara hiyo leo Bungeni mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Andrea Kigwangalla (kushoto) akiwa Bungeni leo mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Dkt. Ashatu Kijaji.
Baadhi ya Wabunge wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
Mwanafunzi wa kidato cha tatu kutoka shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza Getrude Clement akiwa Bungeni leo mjini Dodoma kwa mwaliko wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba ambapo Serikali imetambua na kuthamini mchango wake kwenye utunzaji wa mazingira. Mwanafunzi huyo alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchi, uliofanyika New York Marekani.
Mashududa walihusika katika zoezi la kuchanganya udongo wakati wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964, wakiwa Bungeni leo mjini Dodoma kwa mwaliko wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba ambapo Serikali imetambua na kuthamini mchango wao katika kuuenzi na kuulinda Muungano wa Tanzania.
Mwanafunzi wa kidato cha tatu kutoka shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza Getrude Clement (wa pili kushoto) ambaye alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchi, uliofanyika New York Marekani akiwa na wanafunzi wenzake Bungeni leo mjini Dodoma.
Naibu Spika Dkt Tulia Ackson na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe January Makamba wakiwa katika picha ya pamoja na mashuhuda waliohusika katika zoezi la kuchanganya udogo wakati wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964. Mashuhuda hao walikuja kutembelea Bunge leo Mei 2, 2016.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma)
………………………………………………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma.
Serikali inaendelea kusimamia mazingira na kuhakikisha mifuko ya plastiki inayotumika nchini iwe ni ile inayokidhi viwango vianvyokubalika ili kuondokana na changamoto ya kuzagaa kwa mifuko hiyo katika maeneo mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba alipokuwa akitoa hoja ya wizara yake kuidhinishiwa maombi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Makamba amesema kuwa sababu kubwa ya kusambaa kwa mifuko plastiki inatokana na mifuko hiyo kutolewa bure na hivyo kuchafua mandhari na kuziba mifereji sehemu mbalimbali hali inayosababisha athari kubwa katika mazingira.
“Asilimia kubwa kwenye mito, maziwa na fukwe za bahari imejaa mifuko ya plastiki, hali hii ni hari kwa usalama wa mazingira yetu” alisema Makamba.
Akiwasilisha hotuba yake, Waziri Makamba amesisitiza kuwa mifuko ya plastiki isiyotakiwa kutumika nchini ni ile yenye unene chini ya maikroni 50 ambayo hairuhusiwi kuzalishwa wala kuingizwa.
Kwa mujibu wa maelekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016, Waziri huyo amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imekamilisha kanuni mpya ya mifuko ya plastiki zinazorekebisha viwango vya unene unaoruhusiwa kutoka Maikroni 30 kwenda Maikroni 50.
Waziri Makamba amesema kuwa kanuni hizo tayari zimesainiwa kupitia tangazo la Serikali Na.271 la mwaka 2015 na kutolewa katika Gazeti la Serikali Julai 17, 2015 na kupewa Na. 29.
Kwa upande wake mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16 wa kidato cha tatu anayesoma shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza Getrude Clement ambaye alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchi, uliofanyika New York Marekani amewahimiza Watanzania kutunza mazingira na kufauata maelekezo yanayotolewa na Serikali na wataalamu wa mazingira ili kuyatunza mazingira wanamoishi.
Getrude amesema kuwa amefarikjika kwa kuwawakilisha vijana wa Tanzania na dunia kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi ambapo mataifa 175 yalikutana kusaini makubaliano ya Paris.
Katika kuwahimiza vijana kujenga tabia ya kutunza mazingira, Getrde amewaasa vijana hasa wanafunzi kusimamia sauala la utunzaji wa mazingira wakiwa shuleni kwa kwa kujiunga na klabu mbalimbali ambapo yeye amejiunga na klabu ya “Mali Hai” iliyopo shuleni anaposoma.
Kwa upande wa Watanzania kwa ujumla kwenye utunzaji wa mazingira, Getrude amesema kuwa ni vema wajifunze kutoka mataifa mengine yanavyosimamia utunzaji wa mazingira hasa matumizi ya mifuko ya plastiki.
Mwanafunzi huyo amekaribishwa na kutambulishwa kwa wabunge leo mjini Dodoma kwa heshima ya kuliwakilisha vema taifa wakati wa utiaji saini makubaliano ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki moon alimkaribisha Getrude kwa viongozi hao na kusema “Ni furaha yangu kumualika Getrude Clement ambaye pia ni mwakilishi wa vijana anayeishi Tanzania na anaziwakilisha sauti za vijana”.
No comments:
Post a Comment