Wednesday, May 4, 2016

WAZIRI MWIGULU ATOA HOJA YA KUIDHINISHIWA KWA BAJETI YA 2016/2017 MBELE YA MWALIMU WAKE WA DARASA LA KWANZA.

mw1Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba akitoa hoja kwa Bunge kuidhinisha makadirio na matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017 leo mjini Dodoma huku akishudiwa na mwalimu wake Maria Mnkumbo (hayupo pichani) aliyemfundisha darasa la kwanza na la pili katika shule ya msingi Makunda iliyopo wilaya ya Iramba Mkoani Singida.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma)
mw4Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na mwalimu wake Maria Mnkumbo (katikati) aliyemfundisha darasa la kwanza na la pili katika shule ya msingi Makunda iliyopo wilaya ya Iramba Mkoani Singida mara baada ya waziri huyo kutoa hoja ya Bunge kuidhinisha makadirio na matumizi ya fedha ya wizara yake kwa mwaka 2016/2017 leo mjini Dodoma.  Kushoto ni mke wa Waziri Mwigulu Neema.
mw2Mwalimu msataafu Maria Mnkumbo aliyemfundisha Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba darasa la kwanza na la pili katika shule ya msingi Makunda iliyopo wilaya ya Iramba Mkoani Singida akiwa ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
mw3Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba akiwa na mwalimu wake Maria Mnkumbo aliyemfundisha darasa la kwanza na la pili katika shule ya msingi Makunda iliyopo wilaya ya Iramba Mkoani Singida mara baada ya waziri huyo kutoa hoja ya Bunge kuidhinisha makadirio na matumizi ya fedha ya wizara yake kwa mwaka 2016/2017 leo mjini Dodoma

No comments: