Sunday, June 12, 2016

Breaking newzz--ZITTO KABWE apotea katika mazingira ya Utata


TAARIFA KWA UMMA.

-------------------------------------------------
Tunaujulisha UMMA kwamba Kiongozi wa Chama chetu cha ACT Wazalendo ndg. Zitto Kabwe amekuwa anatafutwa na Polisi tangu jana usiku. Mpaka sasa hatujui Kiongozi wetu yupo wapi na yupo kwenye Hali gani. Askari kanzu wanalinda nyumbani kwake na kwa watu wake wa karibu. Sisi kama chama tunaliambia jeshi la Polisi kuwa lolote litakalotokea kwa Kiongozi wetu wao watajibu kwa umma.


Msafiri Mtemelwa, 

Kaimu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo
-----------------------------------------------------------------------
Hiyo ni moja ya Taarifa za kiongozi wa chama hicho kihusu kupitea kwa ZITTO KABWE tangia Majira mchana na kutokujulikana alipo kwa sasa.

Katika mkutano wa wanahabari mwenyekiti wa chama hicho Mama AANA MGWIRA amesema kuwa anachofahamu kuhusu ZITTO KABWE ni kuwa walitakiwa wakutane katika kongamano Leo kila mtu akitokea kwake lakini Kutokana na kongamano hilo kutokufanyika hawakuonana ila akasema anaamini kiongozi wao yupo salama japokuwa ameonekana kutokuwa na Taarifa za kutosha kumhusu ZITTO KABWE.

No comments: