Saturday, June 4, 2016

Fainali ya Insha Competition kufanyika Jumapili hii ya Juni 5, Mjini Unguja

Insha Competition
Mwanzilishi na mwandaaji wa shindano la Insha Competition, Bwana Omary Amiry Mdogwa akiwa katika hatua ya mchujo wa mashindano hayo hivi karibuni
Jumla ya wanafunzi 20 waliongia katika hatua ya 20 bora wanatarajiwa kushirikii katika shindano la Insha competition lililo andaliwa na The voice of the voiceless Foundation upande wa Unguja, Zanzibar kwa kushirikisha shule za sekondari na kwa wanafunzi wa kidato cha tatu na cha nne.

Kwa mujibu wa waandaaji wa Insha Competition, Bwana Omary Amiry Mdogwa amesema kuwa tayari maandalizi yote yamekamilika na shindano hilo linatarajiwa kufanyika ndani ya ukumbi wa Hotel ya Double Tree by Hilton mjini Unguja kuanzkia saa 3 hadi mchana huku wadau mbalimbali wakialikwa kushuhudia tukio.

Aidha, kwa mwaka huu shindano hilo limedhaminiwa na ComNet Tz , Printplus ,Tropical Air ,Double Tree Hotel, Bomba Fm na wengine wengi.

Majaji ya shindano hilo ni walimu wa shule mbalimbali za Sekondari. Hili ni la mara ya kwanza ambapo jumla ya washiriki walikuwa 120. Katika hatua ya awali hadi sasa walichujwa na kubaki 20 ambao wameingia 20 bora.
Katika fainali hiyo washindi watatu wanatarajiwa kupatikana.
13323983_987464547968537_1156555837_oWanafunzi wakiendelea na Insha Competition

13340440_987463764635282_807664143_oWashiriki wa shindano hilo la Insha Competition katika hatua ya awali kuelekea 20 bora
13332932_987430481305277_3842658232491921440_n
13321131_987462424635416_166142226_oBaadhi ya washiriki wa Insha Competition waliongia 20 wakiwa katika picha ya pamoja

No comments: