Monday, June 13, 2016

HUYU NDIYE ZITTO ZUBERI KABWE-AIBUKA BAADA YA KUWAKWEPA POLISI KWA SIKU MBILI,ASEMA NIPO NJOONI

Baada ya taarifa za kutoweka, Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameibuka leo na kusema yuko salama wa afya huku akilaani mbinu za Jeshi la Polisi kutaka kumkamata kwa siri bila kufuata utaratibu unaotakiwa.

Tangu Jumamosi usiku, vyombo mbalimbali vya habari viliripoti Zitto kutofahamika alikokuwa baada ya simu zake zote kutopatikana huku viongozi wa chama hicho wakihofia kukamatwa na polisi baada ya kubaini njia za uviziaji wa kumkamata nyumbani
kwake.

"Ilikuwa Jumamosi , walikuja nyumbani kwangu wakiwa na magari matatu ila hawakufanikiwa, siwezi kukamatwa kwa `terms' zao ila nitakuwa tayari kukamatwa kwa `terms' zetu na wala siyo kuviziana, kama nina makosa kwa nini wanivizie," amesemaZitto Kabwe na kuongeza; 
''Watu wetu wa Usalama wa Chama walihakikisha kwamba sitakamatwa ili niweze leo kupata fursa kuzungumza na watanzania kupitia nyie wana habari
  ''Hatufahamu Watawala wanaogopa nini mpaka kuzuia mikutano ya wanasiasa

  ''Nasikia Jana Walimkamata Mwenyekiti Mbowe wa Chadema Huko Mwanza kisa eti kawasalimia wananchi, huu ni uvunjwaji na ukiukwaji mkubwa wa utawala wa kidemokrasia
  ''Tunalaani tabia za Kidikteta za Rais Magufuli .Magufuli ameanza na vyama vya siasa kuonyesha Udikteta wake, nawahakikishia akimalizana na Vyama vya siasa atahamia kwenu Wanahabari, Tumkatalie

  ''Ndio maana Magufuli Ziara yake ya Kwanza alifanya Rwanda, tumegundua kuwa alikwenda kujifunza namna ya Kudhibiti Demokrasia na Kuongoza Kidikteta
  ''Hauwezi kupambana na Ufisadi kama haumpi nguvu ya Kiutendaji wa CAGKwa hali Hii anayokwenda Magufuli ajiandae kuwa rais wa term moja kwa sababu watanzania hawataweza kuvumilia kutawaliwa, kuminywa na kuburuzwa .

  ''CCM wamdhibiti Magufuli, na wasipomdhibiti sisi na Watanzania Tutamdhibiti
  ''Hatutakaa Kimya hata kama atatufunga, akimfunga Zitto watazaliwa wakina Zitto wengine, na kwenye hili hatutakaa Kimya, tutasimama kidete mpaka nchi irudi kwenye misingi''
  ''IGP ameagizwa na Magufuli anikamate, lakini hawezi kunikamata bila kufuata utaratibu, hawawezi kunikamata kwa kunivizia, viongozi hatukamatwi kwa kuviziwa viziwa, tumewaonyesha kwamba Polisi wanaweza kutukamata kwa kufuata terms zetu na sio zao

  ''Karibuni kesho saa tisa kwenye Kongamano letu, Hatuwezi kuacha kufanya siasa, lazima tuendelee kufanya siasa, mmehudhuria mikutano yetu hamjaona hata sisimizi amekanyagwa
  ''Wanasema Bajeti imeongezeka kwa 32% ukweli ni kwamba Bajeti imeshuka kwa maana Dola imeporomoka''

No comments: