LIVE-- TANZANIA WOMEN CHAMBER OF COMMERCE (TWCC) KWENYE MAONYESHO YA SABASABA
NI kampuni inayojihusisha na kuendeleza biashara za wanawake wajasilia mali wa Tanzania. TWCC ni shirika lisilotengeneza faida na fedha inayopatikana uzungushwa na higaiwa kama gawio. Pia inajihusisha na vitu vingi kama kutoa mafunzo ya kibiashara kwa wanawake wote,pia wanatumia kuwajengea uwezo wa kutumia mikopo mbalimbali ili kuweza kuendesha biashara zao, kuwapeleka sehemu mbalimbali za maonyesho kama saba saba nane nane na matamasha ya kimataifa ili kuweza kujifunza ushindani wa kibiashara,pia wanasidia wanawake wote hata kama sio wanachama ila kwa upande wa fursa zinatolewa kwa wanachamma kwanza.

TWCC inashirikiana na mashirika mbalimbali ya kiserikali na yasiyo ya kiselikali ili kuweza kupata misaada mbalimbali baadhi ya mashirika hayo ni kama UN woman,CRDB, MNB pamoja na wizara mbalimbali kama vizara ya viwanda na biashara pamoja na wizara inayojihusisha na wanawake.

Ndani ya banda lao lililopo sabasaba kuna mkusanyiko wa wafanya biashara toka mikoa mbalimbali kama, Moshi Arusha Tanga Dar es salaam na mikoa mingine wanachama,na wote wamekuja na biashara tofauti tofauti ikiwa ni kazi za mikono yao wenyewe na baadhi ya bidhaa hizo ni sabuni, dawa za madoa,batiki, mikeka, na bidhaa nyingine nyingi ikiwemo nafaka.

Akizungumza na mwandishi wa Mtandao huu ambao umeweka kambi katika maonyesho ya saba saba Jijini Dar es salaam amesema kuwa Changamoto kubwa walio nayo ni fedha kampuni inakuwa na wakati mgumu kwa kuwa kwenye maonyesho kama hayo inabidi iwafadhili toka mikoa wanayotoka mpaka hapa walipo na pia kuwafundisha pamoja na kuendesha semina jinsi ya kuwasaidia wanawake wengi zaidi na kitu kingine ni kukosa masoko ya uhakika kwa ajili ya wajasilia mali hao.

TWCC inawashauri wanawake Tanzania kuweza  kujiunga ili kuweza kusaidiwa kujipeleka mbele Zaidi pia inawashauri mabinti wadogo kuja kwa wingi na kuachana na dhima ya kuajiriwa ni bora waweze kujiunga huku ili kutimiza ndoto zao. hao yote yamesemwa na MWAJUMA HAMZA Deputy executive director wa TWCC. na anawashuri watanzania wote kuweza kutembelea banda lao lililopo karibu na wizara ya mali asili na utalii kwa kuweza kuwaunga mkono wakina mama wa kitanzania ili kuweza kuwapa uwezo wa kutangaza soko la nyumbani

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.