Sunday, June 26, 2016

MASAUNI AKABIDHI MSAADA WA PAMPU NA KUKAGUA MIRADI JIMBONI KIKWAJUNI

m1Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar  ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi  wa Operesheni  za Kiufundi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar, Maulidi Hassan Khamisi(kulia), bomba za pampu ya maji itakayotumika  kuunganisha mtandao wa maji .Mradi huo una umbali wa kilomita 3.5. ukiwa na lengo la kutatua kero ya maji jimboni hapo.m2Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar  ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kulia), akiangalia mafundi wakiweka tuta barabarani wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa barabara katika jimbo hilo ikiwa na lengo la kutimiza ahadi za ujenzi wa barabara kwa wananchi wa jimbo hilo.m3Mhandisi wa Mradi wa Uwekaji wa Taa za Barabarani katika Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar, Ephantus Mathi (kushoto)kutoka Kampuni ya Central Electrical, akitoa maelezo juu ya mradi huo kwa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia). Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor Salum Jazeera.m4Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar  ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wataalamu  wa Mradi wa Uwekaji  Taa za Barabarani katika Jimbo la Kikwajuni.
m5Mafundi kutoka Kampuni ya Central Electrical wakiendelea na uwekaji wa nyaya za umeme katika moja ya nguzo ya taa katika mitaa ya Jimbo la Kikwajuni ikiwa ni ukamilishaji wa ahadi za Mbunge wa Jimbo hilo, Mhandisi Hamad Masauni.
(Picha na Mpiga Picha Wetu)

No comments: