Monday, June 13, 2016

NI BAJETI KILA KONA-TGNP NAO WAWAKUTANISHA WADAU MBALIMBALI KUIJADILI,PICHA ZA TUKIO HILO ZIPO HAPA

Profesa PROSPER NGOWI kutoka chuo kikuu cha Mzumbe akichambua Bajeti ya serikali iliyosomwa Bungeni wiki Hii Mbele ya wadau mbalimbali waliokusanyika Katika Ukumbi wa makao makuu ya Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam Ambapo Mkutano huo uliwakutanisha wataalam na wadau mbalimbali kwa ajili ya Kujadili kwa pamoja Bajeti ya Tanzania mwaka 2016/2017 na jinsi inavyoweza kumsaidia Mtanzania wa Kawaida
Mkurugenzi mtendaji wa Mtandao wa TGNP Bi LILIANI LIUNDI akifungua kongamano hilo mahususi kwa ajili ya kujadili kwa Pamoja Bajeti ya serikali iliyosomwa na waziri mwenye Dhamana ya Fedha DR PHILIP MPANGO bungeni wiki hii,Katika kongamano hilo Wadau mbalimbali wamepata nafasi na Fursa ya kutoa maoni yao ambao wengi wameendelea kuonyesha wasiwasi wao kautika utekelezaji wa Bajeti hiyo na Jinsi inavyoweza kutumika kumusaidia mtanzania maskini zaidi ya kumkandamiza 

Afisa Programu wa uchambuzi na machapicho kutoka  TGNP MTANDAO Bwana DEOGRATIUS TEMBA akitoa mada mbele ya wadau mbalimbali kuhusu maswala ya bajeti Pamoja na mazingira magumu ya wananchi wanayopata endapo bajeti hiyo haitawafikia wananchi wa Kijijini 
Pichani ni PROFESA MARJONE MBILINYI ambaye ni Member wa TGNP MTANDAO akizungumzakatika ongamano hilo la kujadili bajeti ambapo Yeye alikuwa akitazama sana kuhusu nafasi ya mtoto wa kike katika kufaidika na Bajeti ya Tanzania mwaka huu 
Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam DR VINSENCIA SHALE akifafanua jambo wakati wa kujadili bajeti ya serikali leo ambapo TGNP MTANDAO uliwakutanisha wadau mbalimbali pamoja kujadili nni jinsia gani Bajeti ya mwaka huu inaweza kuwasaidia watanzania walio wengi
PICHA ZA TUKIO HILO NA WADAU MBALIMBALI WALIOSHIRIKI ZIPO CHINI






No comments: