Monday, June 13, 2016

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AAPISHWA NA KUPOKELEWA MAKAO MAKUU YA WIZARA.

mwi1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mwigulu Lameck Nchemba(Mb) kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
mwi2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Charles John Tizeba (Mb) kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
mwi3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba mara baada ya kuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.

indexRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba mara baada ya kuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
mwi5Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba kulia pamoja na kaka yake Mhandisi Adrian Tizeba mara baada ya kumalizika kwa tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam. Mhandisi Adrian Tizeba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Mwanza amerejea rasmi Chama cha Mapinduzi CCM. PICHA NA IKULU
gul1Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh, Mwigulu Nchemba(kulia), na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni, muda mfupi baada ya Rais Dkt. John Magufuli kumwapisha Waziri Mwigulu Nchemba kuongoza wizara hiyo leo.
gul2Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Nchemba(Kushoto), akikaribishwa Makao Makao ya Wizara hiyo na Katibu Mkuu Meja Jenerali Projest Rwegasira.Katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamad Masauni na wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Balozi Yahya Simba.
gul3Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Mawasiliano, Jane Massawe, mara baada ya kupokelewa Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
gul4Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akiweka saini mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi muda mfupi baada ya kuapishwa kwake. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Yahya Simba.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

No comments: